Posts

Showing posts from March 3, 2013

MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI TUZO ZA MWANAMAKUKA KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Image
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwahutubia wanawake na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo  za Mwanamakuka 2013, zilizofanyika sambamba na uksherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana Machi 8,  2013. Picha na OMR Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya hundi ya Sh. milioni 6, mshindi wa kwanza  wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, Aziza Mbogolume, wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika sambamba na kusherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika  Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, na baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki kucheza muziki na msanii wa muziki  wa kizazi kipya, Baby Husna, wakati akitoa burudani kwenye hafla ya kutoa tuzo za Mwanamakuka 2013 zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Wanawake 

YANGA YAICHAPA TOTO AFRICA 1 - 0

Image
 Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete (kulia) akimtoka beki wa Toto Africa, Robert Magandula, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,leo. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Mshambuliaji Nizar Khalfan, aliyeingia kuchukua nafasi ya Jerry Tegete, akitokea benchi katika dakika ya 78.   Hamis Kiiza (katikati) akiwania mpira na mchezaji wa Toto, Mussa Mussa, wakati wa mchezo huo.  Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, akichuana kuwania mpira na Emmanuel Swita, wa Toto, wakati wa mchezo huo. Hamis Kiiza, akiwania mpira na kipa wa Toto, Eric Ngwege, wakati wa mchezo huo.

WAZIRI MKUU WA DENMARK AKUTANA NA KATIBU MKUU WA EAC ARUSHA

Image
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Africa Mashariki (EAC) Dk. Richard Sezibera (kulia) akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark Mh  Helle Thorning Schmidt alipotembelea makao makuu ya jumuiya Arusha,Tanzania.  

Uhuru Kenyatta declared Kenya president-elect

Image
Mr Uhuru Kenyatta and his wife Margaret in a May 20,2012 picture. Mr Kenyatta has been declared Kenya's president-elect after a tightly-contested race. The Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) has declared Mr Uhuru Kenyatta the winner of Kenya's election. The proclamation had been much-anticipated after Mr Kenyatta attained the 50 per cent plus one threshold required following tightly-contested March 4 elections. IEBC chair Isaack Hassan said the election had been the most complex in the country's history, with voters picking six categories of candidates. Kenyans had voted "calmly, patiently, proudly and peacefully in the full glare of whole world," he said. "The commission is satisfied the vote was fair and credible," Mr Hassan said in Nairobi Saturday during his nationally televised address. "I therefore declared Mr Uhuru Kenyatta the duly elected President of the Republic of Kenya." Mr Kenyatt

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI MHARIRI MTENDAJI WA HABARI CORPORATION ABSALOM KIBANDA AFRIKA YA KUSINI

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg,  Afrika ya Kusini leo jioni.Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).Picha na Freddy Maro Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg,  Afrika ya Kusini leo jioni.Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Af

MAMA SALMA AZINDUA KISIMA CHA MAJI KATIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE JIJINI MWANZA

Image
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,kwa msaada wa Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kisima hicho kimegharimu shilingi milioni sabini. wa pili kulia  ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Paschal Mabiti na kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Jaji Mark Bomani na wamwisho kulia ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 7.3.2013.(PICHA NA JOHN LUKUWI) Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua koki ya maji wakati wa kuzindua rasmi kisima cha maji katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure . Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaidiana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Valentino Bangi  kumtwisha ndoo ya maji ndugu Getrude Ndaweka ambaye ni afisa muuguzi katika hospitali ya Sekou Toure wakati wa sherehe za uzinduzi wa kisima cha maji

RAIS KIKWETE AMWANDALIA DHIFA YA KITAIFA WAZIRI MKUU WA DENMARK IKULU

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya kinyago cha ‘Shetani,  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku   Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  akifurahia zawadi ya kinyago cha ‘Shetani’ alichopewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana usiku Ikulu   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonganasha glasi ya kutakiana afya njema na  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt wakiangalia ngoma za utamaduni za kundi la JKT  katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku

TAARIFA: Maendeleo ya Afya ya Kibanda

Habari za jioni wakuu, Muda umekwenda lakini nimeona ni vyema tukashirikishana taarifa fupi tulizopata kutoka Afrika Kusini anakotibiwa Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda kama nilivyoahidi. 1. Tangu walipowasili jana katika hosipitali ya Milpark, Kibanda amekuwa akiendelea na matibabu kwa maana ya kufanyiwa vipimo mbalimbali vikiwamo CT Scan na X Ray hasa kichwani na sehemu nyingine za mwili ambazo zilipata majeraha. 2. Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo, jopo la madaktari wenye ujuzi wa aina tofauti, walikuwa akitarajiwa kukutana ili kusoma taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo, ili kutafsiri maana ya matokeo hayo kisha kutoa mwelekeo wa nini kinafuata au aina ya tiba anayopaswa kupata Kibanda. 3. Taarifa nyingine ni kwamba, imebainika kwamba mfupa laini (fizi) uliopo kati ya pua na mdomo ni kama umekatika. Hii natokana na nguvu na nyenzo walizotumia watesaji kumg’oa meno. Kutokana na hali hiyo ana maumivu makali sana kwenye kinywa chake. 4. Pia imebainika kwamba meno kama sita hivi

WAZIRI MKUU AHAMASISHA UFUGAJI NYUKI

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mizenga  baada ya kutundika mizinga miwili ya nyuki  katika kijiji cha Agondi wilayani Manyoni ili kuhamasisha ugaji wa nyuki na usindikaji wa asali nchini Machi 4,2013. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Vincent Ole Kone. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitundika mzinga wa nyuki ili kuhamasisha ufugaji nyuki na usindikaji wa asali nchini, wakati alipokwenda kwemye kijiji cha Agondi wilayani Manyoni, Machi 4, 2013. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absolom Kibanda, aliyelazwa katika Wodi ya Moi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati akiingia nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPP Regnard Mengi. Picha na OMR Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absolom Kibanda, akionekana jinsi  alivyojeruhiwa.

MH Edward Lowassa Atoa Pole Msiba wa Benson Mollel Jijini Arusha

Image
  Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli-CCM Mh Edward  Lowassa akitoa pole kwa mama mzazi wa Mollel nyumbani kwao Daraja Mbili Arusha Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ametoa pole nyumbani  k wa mjumbe wa baraza kuu la Umoja wa Vijana CCM Benson Mollel aliyefariki katika mazingira ya kutatanisha jana hotelini jijini Arusha. Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa(katikati) akiwa na mwenyekiti wa CCM Monduli(kulia) Ruben Kunei na mjumbe wa halmashauri kuu taifa NEC (kushoto) Mathias Manga

Waziri Mkuu wa Denmark Awasili Tanzania

Image
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt muda mfupi baaday kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni hii   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt wakipokea heshima za nyimbo za Taifa pamoja na saluti ya mizinga 21  katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam   Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake   Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt na mwenyeji wake wakifurahia burudani mbalimbali   Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akipkea shada l maua Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akisalimiana na kinamama waliofurika uwanjani kumlaki. Picha na Freddy Maro

ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN MJINI MAGHARIBI

Image
  Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi na wazee wa  Chumbuni  Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi, alipofungua kituo cha  Mafunzo ya Kazi za Amali,akiwa katika ziara Mkoa huo,(kulia) Naibu  waziri wa Ulinzi Perera Ame Silima,na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abadallah  Mwinyi Khamis,na (kushoto)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame    Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala ya kituo cha kituo cha Mafunzo ya  Kazi za Amali,Chumbuni Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi, kutoka  kwa Katibu wa Chuo Iddi Sheha Makame,alipokizindua kituo hicho akiwa  katika ziara Mkoa huo Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Hassan Ali  Mbarouk,(kulia) akitoa maelezo kwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati alipotembelea kituo kipya cha Umeme huko Welezo alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magha

MKUTANO MKUBWA WA UVCCM ULIVYOFANYIKA JANA MKOANI MOROGORO

Image
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akihutubia kwenye mkutano huo Mmoja wa vijana machachari aliyehama hivi karibuni kutoka Chadema, Mtela Mwampamba akihutubia kwenye mkutano huo. “Vijana Chadema wanawazingua tu, wanawahamasisha kufanya maandamano ili wawapige picha za kwenda kuonyesha  nchi za nje kwa mafariki zao kwa ajili ya kupatiwa mamilioni ya fedha”, anasema Mwampamba kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya UVCCM Kaka Mpokwa. Kama Mwampamba, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Taifa, Juliana Shonza, ambaye amehamia CCM hivi karibuni, akibebwa na vijana wa UVCCM, baada ya ‘kuimwagia razi’ Chadema jukwaani kwenye mkutano huo. Mbunge wa Morogoro, Abdulaziz Mohamed Abood akiongoza msafara wa pikipiki kwenda kwenye mkutano huo Vijana wakiserebuka kwa nyimbo za hamasa kwenye mkutano huo