Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova. Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam , Suleiman Kova akiwaonyesha waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk