Posts

Showing posts from September 15, 2013

Rais Dkt. Kikwete afungua ubalozi wa Heshima San Francisco

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya ubalozi wa heshima(Honorary Consulate) wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kulia ni Balozi wa heshima wa Tanzania jijini San Francisco Mh.Ahmed Issa na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na wapili kushoto ni Mke wa Balozi Mama Sherry Julin Issa.   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Tanzania jijini San FranciscoMh.Ahmed Issa,(wapili kushoto) muda mfupi baada ya kufungua ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na kulia ni mke wa balozi Ahmed Mama Sherry julin Issa.   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani muda mfupi baadaya kufungua ubalozi wa heshima wa Tanzania na kuzungumza nao leo jioni.   Rais Dkt.Jakaya MrishoKikwete akizungumza na baadhi ya

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa Asimikwa Rasmi Kuwa Chifu wa Unyenyembe Mkoani Tabora

Image
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akivishwa vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa Mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo,wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora. Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa  akionyeshwa moja ya kibuyu cha tambiko la wanyamwezi Chifu mkuu wa unyanyembe,Chifu Msagata Fundikira akifanya tambiko muda mfupi baada kumtawaza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa Mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 il

KATIBU MKUU WA CCM ABDURALRAHMAN KINANA AITEMBELEA FAMILIA ILIYOUNGULIWA NA NYUMBA SHINYANGA MJINI NA KUELEKEA SIMIYU

Image
 Wakazi wa kijiji cha Wigelekelo kata ya Masela wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye mkoa huo ikiwa sehemu ya ziara yake inayoanza leo wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.  Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Isanga baada ya kuzindua shina la Muungano.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuchanganya mchanga kwa ajili ya kufyatulia matofali kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha N'hami wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa ajili ya ujenzi wa kijiji cha N'hami wilaya ya Maswa  mkoa wa Simiyu. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya N'humi,wilaya ya Maswa.  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibeba tofali kushiriki na fundi kujenga zahanati ya kijiji cha N'humi wilaya ya Maswa mkoani Simi