Posts

Showing posts from June 2, 2013

HOYCE TEMU AKONGA NYOYO ZA WASHIRIKI WA SEMINA YA HOW TO FIND YOUR DESTINY

Image
Mwendesaji wa semina ya “How To Find Your Destiny”  Hoyce Temu akisikiliza utambulisho kutoka kwa washiriki waliohudhuria semina hiyo ambao baadhi yao ni wajasiriamali, waajiriwa wa serikali, Mentors na wanafunzi wa vyuo. Semina hiyo  imefanyika kwenye Taasisi ya Mara Foundation ya jijini Dar. Pichani juu na chini ni Mwendeshaji wa semina ya “How To Find Your Destiny”  Hoyce Temu aki-share experience ya maisha yake mpaka hapo alipofika baada ya kupitia vikwazo vingi, kuvuka mabonde na malima wakati wa semina hiyo. Pichani juu na chini ni Washiriki wa semina ya “How To Find Your Destiny” wakifuatilia kwa umakini shuhuda na mifano mbalimbali ya maisha iliyokuwa ikitolewa na Mwendeshaji wa Semina hiyo Hoyce Temu(hayupo pichani). Mwendeshaji wa Semina ya  “How To Find Your Destiny”  Hoyce Temu akigawa kitabu chake kinachoelezea historia ya maisha yake kinachoitwa “Nayakumbuka Yote” ambacho kinauzwa katika m...

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA SINGAPORE

Image
Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huoleo Juni 6, 2013. . Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu) kulia. Mojawapo ya vivutio vikubwa katika jiji la Singapore ni hoteli hii ya kitalii na casino iitwayo Marina Bay ambayo kuna jengo la mgahawa  lenye umbo la meli juu ya majengo yake mawili Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji Upya  ya Singapore leo Juni 6, 2013 ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamla...

MWIGULU NCHEMBA AUNGURUMA ARUSHA UCHAGUZI WA UDIWANI

Image
Mh.Mwigulu Nchemba akipokewa na wanachama wa CCM waliojitokeza viwanja vya Shule ya Msingi Erelai kata ya Erelai mkoani Arushahii leo wakati wa kampeni za kumnadi Mgombea Udiwi kwa tiketiYA CCM Mwalim Emanuel Laizer Meya (kushoto)wa wilaya akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya wakati wa mkutanohuo viwanja  vya shule ya msingi Erelai ARUSHA. Mamia ya wananchi wakisikiliza sera za Mgombea wao pamja na hotuba ya Mh.mwigulu Nchemba. Naibu katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba akiomuonesha moja ya vijana waliojeruhiwa kutokana na siasa chafu za vyama vya upinzani.hapa Mwigulu anasisitiza siasa zio vita.Siasa ni amani na utulivu wapuziwe wote wanaohamasisha vurugu hapa nchini Makada wa CCM Juliana shonza na Mtela mwampamba wakifuatilia mkutano huo kwa karibu. Huyu ndiye mgombea wa Udiwani kata ya erelai Arusha mjini.Ndugu Mwalimu emmanuel Laizer.Mgombea huyu kwa tioketi ya CCM ameomba apewe kura za kutosha iliawaletee maendeleo wanakata ya Erelai.Amesisitiza amesha...

SIMANZI,BAADA YA HADIJA KOPA KUSIKIA MME WAKE KAFARIKI HALI IKAWA HIVI

Image
Khadija Kopa akilia kwa uchungu hata kushindwa kutembea mwenyewe. Dah sina hata la kusema. Pole sana mama Mwenyezi Mungu akutie Nguvu katika kipindi hiki kigumu Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kuapanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri kutokana na ugonjwa. Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana. Picha kwa hisani ya zeddyblog

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASIMU YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Waziri Mkuu,  Mizengo Pinda, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.   Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu wa Kwanza wa  Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya  Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.Picha na Ofisi ya Makamu  wa Rais Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu Mwenyekiti  wa Jukwaa la Wahariri, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karim...

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ACHARUKA KASI NDOGO YA UJENZI WA BARABARA RUKWA

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI   WAZIRI MKUU Mizengo Pinda jana jioni (Jumamosi, Juni Mosi, 2013) alilazimika kufanya ziara ya ghafla kwenye kambi ya wajenzi wa barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni ili kupata maelezo ni kwa nini kazi hiyo inasusua na haionyeshi kuendelea. Waziri Mkuu ambaye alikuwa akitoka Namanyere, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani  ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Rukwa alilazimika kusimama kwenye kambi hiyo ya wajenzi iliyopo Paramawe, wilayani Nkasi . Kampuni inayohusika na ujenzi wa barabara hiyo ni China Hunan Construction Engineering Group Corporation (CHCEG) na gharama za mradi huo ni sh. bilioni 82.8/- ambapo hadi sasa kiasi cha sh. bilioni 16.37 kimekwishatolewa na Serikali kwa mkandarasi huyo. Barabara hiyo ya kutoka Kanazi kupitia Kizi hadi Kibaoni ambayo ina urefu wa km. 76.6,  ilianza kujengwa Juni 2009 na ilipaswa kuwa imekamilika Machi 20, mwaka hu...

ALICE ISACK ASHINDA REDD'S MISS DAR CITY CENTER 2013

Image
Mshindi wa Redd's Dar City Center 2013, Alice Isack akipozi kwa picha mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika shindano lililofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar Es Salaam   Mshindi wa Redd's Dar City Center, Alice Isack (katikati) akiwa na mshindi wa pili, Clarah Paul (kulia) na mshindi wa tatu, Fatma Hussein (kushoto) katika shindano lililofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar Es Salaam  Warembo waliofanikiwa kuingia katika hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja.  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kulia) akiwauliza maswali warembo walioingia 5 bora.   Mshindi wa Redd's Dar City Center, Alice Isack (katikati) akiwa na mshindi wa pili, Clarah Paul (kulia) na mshindi wa tatu, Fatma Hussein (kushoto) katika shindano lililofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar Es Salaam. Mkoni ni moja ya zawadi zao.  Redd's Miss Tanzania 2012 pamoja na Mshindi wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce...

SALSHIA ISDORE AIBUKA MSHINDI REDD'S MISS GEITA 2013

Image
Mshindi wa taji la Redd’s Miss Geita 2013, Salshia Isidore (katikati) akiwa mwenye furaha wakati wa kupiga picha ya pamoja na warembo wqenzake Stella Magerezi (kulia) aliyeshika nafasi ya pili na Mshindi wa tatu wa shindano hilo, Nurieth Rashid. Salshia aliwashinda warembo wenzake 12 waliokuwa wakiwania taji hilo pamoja nae.  Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja.  Wanyange walioshiriki shindano la Redd's Miss Geita 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jukwaani. Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoani Geita, Vicky Kamata (kulia) akitoa nasaha zake kwa washindi na warembo wote walioshiriki shindano hilo.