Posts

Showing posts from September 2, 2012

Diamomd apata muwaliko wa Dinner na Missy Temeke Washington DC

Image
Baada ya show ya kukata na shoka Missy Tameke watoa mualiko wa Dinner kwa Muimbaji wa Kizazi kupya Diamomd pamoja na kundi lake la Safi. Mwana muziki wa kizazi kimpya Diamomd akiwa na kundi la safi wakipata picha ya pamoja na Missy Tameke pamoja na Salma Jay Jay, kwa ajili ya kujianda na Dinner iliondaliwa Missy Tameke. Missy Tameke pamoja, Salma Jay Jay pamoja na  Diamomd, wakipata picha ya pamoja kwenye ddinner ya pamoja iliofanyika jana Usiku wa Sept 3. 2012. Kundi zima la mwana muziki wa kizazi kimpya Diamomd wakipata Dinner ya pamoja na Missy Tameke. baada ya show yao iliofanyika Sept1,2012     Missy Tameke kulia  pamoja, Salma Jay Jay kushoto wakiwa kwenye High table wakiwaza jambo kabla ya kupata dinner ya pamoja. Missy Tameke  pamoja na rafiki zake wakinyanyua kilasi za upendo baada ya kumaliza Dinner ya pamoja Mwana muziki wa kizazi kimpya Diamomd akipata picha ya pamoja na Kundi Zima la Mabanati wa Maryland. US Cheif  w...

Mazishi ya Mwandishi Daud Mwangosi Kijijni Kwao Rungwe

Image
  Mke wa marehemu akiaga Mh. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mke wake  Picha zote kwa hisani ya  http://mbeyayetu.blogspot.com Dr. Wilbroad Slaa na Profesa Mark Mwandosya.  Kwenye msiba wa mwandishi Daud Mwangosi. Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog.

ZITTO KABWE 'AANIKA' UTAJIRI WAKE

Image
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe amejibu tuhuma zinazoelekezwa kwake kwa kusema "Sijawahi kuwa na nyumba wala kiwanja hapa Dar wala Dodoma isipokuwa nyumbani Kigoma, huko nina nyumba vya vyumba viwili tu ambayo niliijenga wakati wa uchaguzi baada ya wazee kunishauri kuwa siyo vizuri kuendelea kutumia nyumba ya baba yangu.   Ninapaswa kuwa na kwangu. Labda kuna shamba la hekari tatu na nusu nililopewa na bibi yangu liko Kigamboni eneo la Mbutu, sijaendeleza hadi sasa, lipo tu. Lakini pia ieleweke kuwa nina uwezo wa kujenga kama Mbunge, wabunge wenzangu wengi tu wanajenga, mimi ninashindwa kwa sababu ya majukumu yangu ya kifamilia. Nimeshasikia sana watu wanazungumza ninajenga ghorofa kubwa Dodoma na baadhi ya watu wanaiita sehemu hiyo kuwa ni kwa Zitto sina hata kiwanja Dodoma, uzushi mtupu wa maadui zangu kisiasa".  Akizungumzia Utitiri wa magari ya kifahari anayodaiwa kuwa nayo anasema "Watu wanaishi maisha ya kufikirika sana, hayo magari wa...

DKT. SLAA, ARCADO NTAGAZWA NA WANANCHI WAHANI MSIBA WA DAUDI MWANGOSI.

Image
  Mti huu ni kwa ajili ya kumbukumbu ya Daudi Mwangosi kututoka kimwili lakini angali nasi kiroho hadi tutakapoungana naye tena. Nyumbani kwa marehemu Daudi Mwangosi, TRM, Mtwivila, Iringa. Itika Mwangosi, mkewe marehemu Daudi Mwangosi. Marehemu Daudi ameacha mke na watoto wanne, wa mwisho ana umri wa miaka miwili. Mwana wa Daudi Mwangosi akimkumbatia Dkt. Wilbrod Slaa. Anayeangalia kulia ni Ndg. Arcado Ntagazwa. Picha zote ni kutoka   MjengwaBlog.com

ZIARA YA VIONGOZI WA CHADEMA DMV

Image
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Ndg Freeman Mbowe akihutubia Watanzania waishio Washington DC, Marekani. Mbunge wa Mbeya Mjini Ndg Joseph Mbilinyi akihutubia Watanzania Waishio Washington DC, Marekani. Mwenyekiti wa Chadema DMV Ndg Cosmas Wambura akihutubia katika mkutano wa Chadema Washington DC. Katibu wa Chadema DMV Ndg Isidory Lyamuya akihutubia katika Mkutano huo. Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema DMV Ndg Mariam Khamis akiwa katika mkutano wa Chadema DMV. Katibu wa Baraza la Wanawake Ndg Baby Mgaza akihutubia katika mkutano huo. MC Sunday Shomari akiongea mawili matatu katika Mkutano wa Chadema DMV. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Chadema DMV Ndg Kalley Pandukizi akitoa Risala ya Historia ya Tawi la Chadema DMV. Pichani Viongozi wa Chadema DMV wakiwa katika mkutano Washington DC. Baadhi ya Watanzania waliojitokeza kwenye mkutano wa Chadema DMV. chademablog.blogspot.com

Vurugu Iringa zaua mwandishi

Image
Marehemu Daud Mwangosi Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi Askari Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU),wakimsulubu mtu anayedaiwa kuwa ni Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten Iringa,Daud Mwangosi katika vurugu zilizotokea kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema kwenye kijiji cha Nyololo,Mufindi jana.Katika vurugu hizo mwandishi huyo aliuawa kwa kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu. Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake. (Picha zote na Francis Godwin) Polisi waua tena kikatili KATIKA hali inayoonyesha watawala wamedhamiria kuigeuza nchi hii dola ya kipolisi, jana Jeshi la Polisi liliua mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, aliyekuwa anaripoti habari za ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani hapa. Habari za a...

Serengeti Fiesta 2012 yatikisa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Image
Ni kama vile wanashindano kukatika lakini hapa ilikuwa show ya wacheza filamu Wema Sepetu (kulia) na Aunt Ezekiel wakiserebuka Ndombolo. katika jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 jijini Mwanza. JB akitoa hela katika waleti yake akitishia kuwatunza Wema na Aunt Ezekiel waliokuw wakicheza. Msanii wa Filamu Ray Kigosi akifanya vitu vyake kama Suoer Nyamwela. Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti kutoka Clouds Media Group Bwa. Ruge Mutahaba akisoma namba ya mshindi aliyejishindia gari aina ya Vits ambazo zimekuwa zikitolewa  na kampuni ya Push Mobile katika mchakato mzima wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Kati ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile Bwa,Rugambo Rodney na shoto ni mmoja wa wakilishi wa bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha Bwa.Bakari Maggid wakishuhutia tukio hilo usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.Mshindi wa gari hiyo aina ya Vitz alitajwa kuwa ni Bahati Joseph,mkazi wa jiji la Mwanza,mjasilia mali. Baadhi ya mashabiki wakiwa wa...