Posts

Showing posts from November 18, 2012

DK. SHEIN ZIARANI VIETNAM

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akisalimiana na Makamo wa Rais  Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,alipowasili Ikulu nchini Vietnam,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.[Picha na Ramadhan Othman Vietnam.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakipokea mashada ya mauwa kama ni Ishara ya  ukaribisho katika Ikulu ya Vietnam,alipofika kwa mazungumzo na  Makamo wa Rais wa  Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.[Picha na Ramadhan Othman Vietnam.] Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwamamwema Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais wa  Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,alipowasili Ikulu nchini Vietnam,alipofuatana na Rais wa Zanzibar katika ziara Rasmi ya Kiserikali Nchini Vietnam ya wiki moja.[Picha na Ramadhan Othman V...

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWASILI MKOANI KATAVI TAYARI KWA UZINDUZI RASMI WA MKOA HUO

Image
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutegwe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda leo mchana kwa ajili ya kushiriki katika shughuli ya uzinduzi rasmi wa mkoa huo, utakaofanyika siku ya jumapili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda, mkoa huo utazinduliwa rasmi kwa ving’ola na Mh. Dkt. Gharib Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania anayetarajiwa kuwasili kesho mjini Mpanda tayari kwa ajili ya uzinduzi huo. Waziri Mkuu Mizengo Pinda viongozi mbalimbali wa CCM baada ya kuwasili mkoani Katavi leo mchana  katikati ni Waziri wa Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rtengwe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na  Mbunge wa Mpanda  Mjini, Said Arfi ( Chadema )  mara baada ya kuwasili mjini Mpanda leo Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe kwa ajili ya kukagua vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege wa Mpand...

KINANA AKIHUTUBIA MAELFU YA WATU GEITA JIONI HII

Image
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa mpira, mjini Geita mkoani Geita, jioni hii, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya mikoa minne kujitambulisha kwa wanachama na kukagua uhai wa chama ngazi za mashina na matawi na kusimamia na kueleza utekelezaji wa ilani ya Chama. (Picha na Bashir Nkoromo) Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu, Geita, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mkoani Geita. Jumla ya leseni 21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji hao baada ya kutolewa na serikali ili kuwwezesha wachimbaji wadogo nao kunufaika na m,adini badala ya wachimbaji wakubwa tu. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizindua shina la wakereketwa wa CCM la wajasiriamali watengeneza fenicha katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, jana. Nape aliwapa pia ,msaada wa sh. milioni moja kwa ajili ya wajasiriamali hao kukuza shughuli zao. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtuz...

Bakhresa second richest man in East Africa

Image
 Our very own super businessman Said Salim Bakhresa  is the second wealthiest person in East Africa, with $520 million (Sh832 billion) to his name. Mr Bakhresa, whose business empire spans the East and Central African region, is at position 30 out of 40 in Africa. The self-made billionaire, 63, has interests in grain milling, beverages, packaging, ferry services and petroleum trading. His Bakhresa Group manufactures the popular Azam brand of food products. The annual ranking is compiled by the influential American publication, Forbes Magazine and was released yesterday. “The sales volume of Bakhresa Group are $800 million (Sh1.3 billion) and, in fact, the group is also the largest producer of wheat flour in East and Central Africa with daily capacity of 3,200 metric tonnes,” the magazine reports. In East Africa, the wealthiest entrepreneur is Ugandan businessman Sudhir Ruparelia with a net wealth of $900 million. He is the 18th richest person in Africa. The 56-year-old...

TID NDANI YA MALAYSIA

Image

MBEKI MGENI RASMI MAJADILIANO YA UONGOZI AFRIKA DAR ES SALAAM LEO

Image
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akifafania jambo wakati wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya. Mbeki alikuwa Mgeni Rasmi katika mdahalo huo.  Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo, ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo jijini Dar es Salaam leo.  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja, akizungumza katika mdahalo huo.  Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akikiwa mwenye tabasamu wakati Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na cha...

Bakhresa akamata nafasi ya 30 katika orodha ya watu matajiri 40 barani Afrika – Forbes

Image
Bakhresa (kulia) alipokuwa akisalimiana na rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein Orodha ya jarida la Forbes la watu 40 matajiri zaidi barani Afrika imetupa jibu la ‘uhakika’ nani ni mtu tajiri zaidi kuliko wote nchini Tanzania. Si mwingine zaidi ya Said Salim Bakhresa ambaye amekamata nafasi ya 30 kati ya matajiri 40 wa barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 520 hadi kufikia November, 2012. Bakhresa ana historia ya pekee kwa kuacha shule akiwa na miaka 14 na kujiingiza kwenye biashara ndogo ndogo ikiwa pamoja na mgahawa na biashara ya unga wa kusaga. Leo hii Bakhresa Group imeajiri zaidi ya watu 2,000 na ni kampuni kubwa zaidi Tanzania. Bidhaa zake zina umaarufu mno nchini na nje ya nchi ambazo ni pamoja na unga, vinywaji, ice cream, usafiri wa meli na mafuta miongoni mwa nyingine. Kampuni ya Bakhresa ni wazalishaji wakubwa zaidi wa unga wa ngano Afrika Mashariki na kati ambayo huzalisha kiasi cha 3,200 za tani za metric. Kampuni yake huendeshwa na w...

KINANA,NAPE,KHATIB WATUA MTWARA, WANANACHI WAWAPOKEA KWA SHANGWE

Image
Viongozi wa Juu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahaman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Mnauye na Katibu wa Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatib wamewasilili mkoani Mtwara leo kwa ziara maalum ya kuimarisha chama hicho. Pichani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara,  Mohamed Sinani akiwapokea viongozi hao katika Uwanja wa ndege wa Mtwara. Maandamano ya pikipiki ya wanachama na wafuasi wa CCM Mkoani mtwara yakiongoza msafara wa Viongozi hao kuelekea Ofisi za CCM Mkoa wa Mtwara.

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA IRAN NA CANADA, AONANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS ALI BONGO WA GABON

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Iran nchini Mhe Mehdi Agha Jafari leo Novemba 21, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Iran nchini Mhe Mehdi Agha Jafari baada ya kupokea hati zake za utambulisho leo Novemba 21, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Canada nchini Mhe Alexandre Leveque leo Novemba 21, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Mhe Alexandre Leveque leo Novemba 21, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Iran nchini Mhe Mehdi Agha Jafari baada ya kupokea hati zake za utambulisho leo Novemba 21, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Canada nchini Mhe Alexandre Leveque baada ya kupokea hati zake za utambulisho leo Novemba 21, 2012 Ikulu ...

MABILIONI YA USWISI – TUSIGEUZWE MAZEZETA ;ZITTO KABWE

Image
Jumanne tarehe 20 Novemba 2012, baadhi ya vyombo vya habari vimebeba habari zinazohusu matamshi ya Waziri wa Utawala Bora ndugu George Mkuchika kuhusu sakata ya mabilioni ya Uswisi. Waziri amesema kwamba Serikali ya Uswisi inataka majina ya Watanzania walioficha fedha huko ndio waweze kusaidia uchunguzi. Habari kama Hiyo, yenye maudhui na malengo hayo hayo iliandikwa na Gazeti la The Guardian on Sunday la tarehe 18 Novemba 2012. Nimeona ni vema nitoe kauli yangu rasmi kuhusu suala hili. Lengo ni kuweka rekodi sawa juu ya Azimio la Bunge na kwamba Serikali inapaswa kutekeleza Azimio na sio kutoa kauli tata za kukata tamaa. Moja, Suala hili japo sio jipya lakini limeandikwa kama ni jambo jipya. Suala la Serikali ya Uswisi kutaka majina lilisemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati akichangia hoja binafsi niliyowasilisha Bungeni na pia wakati akileta maombi yake ya kuiondoa hoja ambayo yalikataliwa na Bunge. Kama sio sababu mpya ni kwanini imeibuka upya na kwa kasi? Ni wazi Serik...

SHEREHE ZA MAPOKEZI YA M/KITI NA SEKRETARIETI MPYA YA CHAMA

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi akiingia katika viwanja vya mnazi mmoja. Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akivalishwa skafu na kiongozi wa Chipukizi wa Mkoa wa Dar es salaam. Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa na sura za furaha na bashasha katika sherehe hizo za mapokezi.