MAJIBU YA HALIMA MDEE KUHUSU KUSHUKA KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia” inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo” . Mdee aliongezea kusema hii yote inachangiwa na mipango ya serikali iliyowekwa kwa kiwango kikubwa sana cha fedha kushindwa kutekelezeka au kusimamiwa ipasavyo ili yaweze kutekelezeka na kutolea mfano wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari. (MMES II) ambao serikali ilitenga Shilingi bilioni 200 wakati huo kiwango cha ufaulu daraja la kwanza hadi la tatu ukiwa 37% ikiwa na malengo kiwango kipande