MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA MKOA WA RUKWA


IMG_1951Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo tarehe 25.2.2013.
IMG_1969Akiwa amevalia vazi la asili la akina mama wa kabila la Wafipa, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anashiriki kucheza ngoma ya kabila hilo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga tarehe 15.2.2013.
IMG_2175Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi shina la wakereketwa la kikundi cha akinamama cha Upendo kilichoko katika makao makuu ya wilaya ya Kalambo katika mji wa Matai tarehe 26.2.2013. Akinamama hao wapatao kumi hujishughulisha na kazi ya kukamua mafuta ya alizeti. 
IMG_2302Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akipokewa kwa shangwe na wananchi wa mji wa Matai waliofurika katika eneo la soko jipya mjini hapo ili kushiriki katika sherehe ya kukabidhi pikipiki kumi kwa ajili ya watendaji wa vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi tarehe 26.2.2013.
IMG_2529Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi funguo za pikipiki Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Ndugu Paza Mwamlima kwa ajili ya vituo vya afya vya mkoa huo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Pikipiki hizo zimetolewa na kampuni ya Waterrids. 
IMG_2631Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amembeba mtoto Emma, mwenye umri wa miezi minne na nusu, mtoto wa Maria, ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa mkono na watu wasiojulikana wakati walipovamia nyumbani kwake tarehe 10.2.2013. Maria ni mke wa tatu wa Bwana Gabriel Yohana ambaye siku ya tukio hakuwepo nyumbani kwa Maria wakati watu hao walipomvamia.
IMG_2685Mbunge wa zamani wa Kwela Ndugu Chrisant Mzindakaya akishiriki kucheza ngoma ya utamaduni ya kabila la Wafipa wakati  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipotembelea hospitali ya Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya tiba vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba.
IMG_2754Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013. Vifaa hivyo vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani na vina thamani ya shilingi milioni mia saba.
IMG_2923Mke wa Rais Mama Salma Kikwete hayupo pichani  akiongea na wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga waliokusanyka katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Theresia tarehe 26.2.2013
PICHA NA JOHN LUKUWI WA MAELEZO

Popular posts from this blog

MH. AMANI ABEID KARUME AFUNGUA SKULI YA DONGE ZANZIBAR