Posts

Showing posts from November 11, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGA MKUTANO WA MAJAJI ARUSHA LEO

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala ya Waheshimiwa majaji toka kwa muwakilishi wao, Jaji Dkt Fauz Twalib, wakati wa kufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo Novemba 16, 2012 Rais Jakaya Kikwete akikufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo Novemba 16, 2012 Rais Jakaya Kikwete akikufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo Novemba 16, 2012.Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Nhe. Magesa Mulongo Jaji Mkuu  Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Sheria Mhe Mathias Chikawe, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi Mhe Fakih Jundu ( PICHA NA IKULU) Waheshimiwa majaji wakimsikilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo Novemba 16, 2012.

KINANA ARIPOTI KAZINI, OFISI ZA LUMUMBA DAR

Image
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijinbi Dar es Salaam, aliporipoti rasmi kazini kwenye ofisi hizo leo asubuhi. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliporipoti leo ofisini, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Minister Membe hosts EU-Tanzania Political Dialogue

Image
Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation in brief talks with H.E. Filiberto Cerian Sebregondi, Ambassador and Head of European Union Delegation in Tanzania.  Hon. Membe hosted the political dialogue the European Union delegation in Tanzania that was held today at Karimjee Hall in Dar es Salaam. Hon. Membe (right) opens a political dialogue meeting between Tanzania-European Union.  Left is H.E. Filiberto Cerian Sebregondi, Ambassador and Head of the European Union Delegation in Tanzania during the Tanzania-EU political dialogue held earlier today in Karimjee Hall in Dar es Salaam. A Political Dialogue between Tanzania-EU in session at Karimjee Hall in Dar es Salaam.  H.E. Mrs. Diane Corner, the British High Commissioner to the United Republic of Tanzania gives her comments on recent events of religious demonstrations in Tanzania Mainland and Zanzibar.  Left is H.E. Johnny Flento, Ambassador of Denmark to the United Republic

RAIS AWASILI ARUSHA, VIONGOZI WA DINI WAMPONGEZA NA KUMUOMBEA MAFANIKIO ZAIDI

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiombewa dua na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro leo Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro jioni leo Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha Dua za kumuombea Rais Jakaya Kikwete zikiendelea Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili mkoani Arusha jioni ya leo.

MWENYEKITI WA CCM TAIFA, JAKAYA KIKWETE ATANGAZA SEKRETARIETI MPYA YA CCM, KINANA KATIBU MKUU

Image
 Abdulrahman K i nana-Kat i bu Mkuu wa CCM, Ta i fa.  Mw i gulu Nchemba-Na i bu Kat i bu Mkuu (Bara)  Vua i Al i Vua i -Na i bu Kat i bu Mkuu (Zanz i bar) Nape Nnauye, abak i a kat i ka Nafas i yake ya Kat i bu wa I t i kad i na Uenez i . Asha-Rose M i g i ro- Kat i bu wa NEC, S i asa na Uhus i ano wa K i mata i fa.   Zak i a Meghj i -Kat i bu wa NEC, Uchum i na Fedha. Muhamed Se i f Khat i b, Kat i bu wa NEC, Ogana i zeshen i .

HII HAPA TREIN YA KISASA ALIYOZINDUA RAIS KIBAKI MJINI NAIROBI.

Image
Trein ya kisasa iiliyozinduliwa Kenya inavyoonekana kwa ndani. Viongozi wakenya katika uzinduzi wa Trein mpya Rais Kibaki ikiteremka katika Trein mjini Nairobi Treni ya kwanza ya aina yake imezinduliwa tangu Kenya kujipatia uhuru mwaka 1963. Rais Kibaki aliyefungua rasmi kituo cha Syokimau na alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuipanda treni hiyo.  Kituo cha treni cha Syokimau ni cha kwanza cha aina yake nchini Kenya, kikiwa na mashine za elektroniki zinazokagua vyeti vya usafiri, pamoja na skirini kubwa ambazo zinatangaza safari za treni. Kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria sabini pamoja na miamoja na ishirini watakao simama.  Treni hiyo inanuiwa kupunguza msongamano wa magari mjini Nairobi ambao ni mojawapo ya miji unaokuwa kwa kasi barani Afrika ukiwa na watu zaidi ya milioni tatu.

‘Kwenda Mwanza sasa kwa Sh 32,000 kwa ndege’

Na Gabriel Mushi, Dar es Salaam WAKAZI wa Mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza, wanatarajia kufaidi zaidi usafiri wa anga baada ya Shirika la Ndege la Fastjet kuzindua huduma zake nchini kwa gharama nafuu ya Sh 32,000 kutoka Dar es Salaam kwenda katika mikoa hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa mauzo ya tiketi za safari hizo, Ofisa Mkuu wa Masoko wa shirika hilo, Richard Bodin, alisema wakazi wa mikoa mingine watapata huduma hiyo kila itakapowezekana. Alisema kwamba, shirika hilo limekuja kuwekeza kwa mara ya kwanza katika Bara la Afrika na kuchagua Jiji la Dar es Salaam ili kukuza masoko na kurahisisha usafiri kwa wakazi wake. “Uzinduzi huo wa tiketi ni hatua muhimu katika juhudi za kampuni kuwezesha usafiri wa ndege kwa Watanzania kwa sababu wapo wengi ambao awali walikuwa hawamudu gharama za safari za ndege. “Kwa usafiri wa anga kutoka Dar es Salaam kuelekea Kilimanjaro na Mwanza zitakuwa ni Dola 20 za Marekani sa

Vigogo Uhamiaji watiwa mbaroni, Mmoja akutwa na mil 700

Na Upendo Mosha, Moshi MAOFISA wawili wa ngazi za juu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, wanashikiliwa na kuhojiwa kwa muda wa saa 12 na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani hapa. Maofisa hao walikamatwa juzi asubuhi, wakiwa ofisi za uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro na kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali, ikiwamo matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa fedha za umma. Taarifa kutoka ndani idara hiyo, zinasema maofisa hao wenye cheo cha Naibu Kamishina wa Uhamiaji (DCI), baada ya kukamatwa, walipekuliwa hadi nyumbani kwao. Akizungumza na MTANZANIA, Ofisa Uhusiano Idara Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Kisaka, alikiri kushikiliwa kwa maofisa na kusema hajui sababu zilizopelekea kukamatwa maofisa hao. Hatua ya kukamatwa na kuhojiwa kwa viongozi hao, imekuja miezi michache baada ya tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emanuel Nchimbi, kukamilisha uchunguzi wake kuhusu uwepo wa vibali feki. Habari zinasema, baadhi y

Walter Chilambo ndiye kinara wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),

Image
Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri  (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar) Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi wa shindano hilo,lililofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee, juzi usiku. Baadhi ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, na jaji mkuu wa Shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), akiwa amemkumbatia mshindi wa shindano hilo Walter Chilambo ndani ya ukumbi wa Diamond,Chil