Posts

Showing posts from December 23, 2012

MH. LOWASSA ASHIRIKI IBADA YA SIKUKUU YA KRISMAS VISIWANI ZANZIBAR

Image
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiungana na Wakristo wengine kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika juzi kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar. Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa salaam za Xmas kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar mara baada ya ibada ya Sikukuu hiyo juzi.Mh. Lowassa yuko visiwani humo kwa mapumziko ya sikukuu hiyo,ambapo amewataka watanzania kusherehekea sikukuu hizi za krismas na mwaka mpya kwa amani na upendo huku tukilinda umoja na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA RASMI KITUO CHA POLISI CHA KIBOJE ZANZIBAR

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliminana na maofisa wa Usalama wa Wilaya ya Kati, wakati alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kufungua rasmi Kituo cha Polisi cha Kiboje, kilichpo Mkoa wa Kusini Unguja leo. PICHA NA OMR   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala na Kamishina wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakifunua kwa pamoja kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba...

SAID NOOR ABDULKADIR NA KUTEMBELEA KITUO CHA MAFUNZO YA KOMPYUTA CHA CHWAKA, MKOA KUSINI UNGUJA LEO

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakimsalimia Mzee Said Noor Abdulkadir, wakati alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake, Tunduni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, jana Desemba 23, 2012. Mzee huyo anasumbuliwa na maradhi ya mguu kwa muda wa miaka 13.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka na wananchi wa kijiji hicho, wakati alipofika katika kituo hicho leo Desemba 24, 2012 kwa ajili ya kujionea maendeleo ya kituo hicho, akiwa ameongozana na mkewe Mama Asha Bilal.  Sehemu ya Kompyuta zilizopo katika Kituo hicho cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka, Hamis Himid Ramadhan, wakati alipotembelea k...

RAIS KIKWETE ACHANGIA SHILINGI MILIONI 30 KWA MRADI WA KULEA NA KUHIFADHI MBWA MWITU KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI, MKOANI MARA

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  wakielekea kwenye sehemu ya boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu muda mfupi kabla ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. (PICHA NA IKULU) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  akikata utepe katika boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu  kuashiria rasmi kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012 wakiwa nje ya  boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu akishuhudia kuach...

Mh Waziri Mkuu akiwa Katika ziara ya kuhimiza maendeleo jimboni Katavi

Image
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anapata maelezo kutoka kwa mtalamu wa Tanesco makao makuu Eng. Tumaini Temu kuhusu jinsi jenereta walil lifunga linavyofanya kazi katika kuzalisha umeme katika kijiji cha Kibaoni.kushoto kwa waziri mkuu ni tekinisheni  wa Tanesco Bibi.Salama Mpera. Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anakagua kibanda kilichojengwa kwa ajili ya kuweka jenereta la kufua umeme katika kijiij cha Kibaoni Katavi   Mh.waziri mkuu yupo katika ziara ya kukukagua shughuli za maendeleo na mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya kijijini kwao Kibaoni Katavi. Mh.Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika shamaba lake katika kijiji cha Kibaoni Katavi akiangalia mahindi yalivyostawi. Bwana Godfrey Pinda ambaye ni mdogo wa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anamwelezea Waziri Mkuu kuhusu anavyolima kilimo cha mananasi minazi katika shamba lake katika kijiji cha Kibaoni Katavi  Waziri mkuu yupo katika jimbo lake la Katavi katika kukagua shughuli za maendel...