Posts

Showing posts from March 15, 2015

EU WAMPA TUZO MAMA HELEN- KIJO BISIMBA‏

Image
Umoja wa Ulaya umemtunuku Mama Helen Kijo- Bisimba (pichani) kutokana na mchango wake kwa ajili ya kutetea na kulinda haki za binadamu nchiini. Tuzo hiyo, ilitolewa juzi na EU siku ya Jumanne wiki hii jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Maendeleo Ulaya 2015. Balozi wa Umoja wa Ulaya bwana Filberto Sebregondi alitoa tuzo hizo na kusema kuwa lengo lake ni kusimamia haki kwenye masuala ya kiulimwengu ikiwemo kupambana na umasikini na kuhamasisha raia kujihusisha na maendeleo. Wengine waliotunukiwa tuzo katika hafla hiyo pamoja na Mama Bisimba ni wanamziki Keisha Saban, Fareed Kubanda (FID Q), na Balozi Mpungwe, pamoja na Paul Ndunguru ambae ni msanii na mchoraji. EU imekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu hususani ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ikiwemo vitendo vya ukeketaji, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe. Vilevile, EU imekuwa mstari wa mbele kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kupinga adhabu ya ...

MHESHIMIWA WILLIAM LUKUVI KWENYE ZIARA LONGIDO ARUSHA

Image
Waziri   wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Williama Vangimembe Lukuvi jana alifungua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido na kuwataka wananchi kununua nyumba hizoili NHC iweze kujenga zingine kusaidia Wilaya hiyo kupata makazi bora. Picha zote na Muungano Saguya- Longido, Arusha Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua maandalizi ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido, Arusha kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi kufanya ufunguzi huo jana. Hizi ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa na NHC Wilayani Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi. Ufunguzi wa nyumba hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisalimiana na wafanyakazi wa NHC waliokuwa wamejipanga kumpokea Waziri Lukuvi kufungua nyumba za gharama nafuu zi...

WAZIRI MKUU KUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI JAPAN

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa. Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,Machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa. Waziri Mkuu, MizengoPinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Japan, Bw. Masahito Kawashima kabla ya kuzungumza na ujumbe wa wawekezaji wa Kijapan kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo Machi 17, 2015. Waziri Mkuu, MizengoPinda akisalimian na Mwenyekiti w...

ALI HASSAN MWINYI MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU

Image
RAIS Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ameombwa kuhudhuria kwa mara nyingine katika Tamasha la Pasaka linaloadhimisha miaka 15 mwaka huu. Mwinyi ndiye mgeni muasisi  wa tamasha hilo ambako kwa mara ya kwanza alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la mwaka 2000. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama anapenda rais huyo mstaafu ahudhurie siku hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi muasisi ambaye pia ni mlezi, hivyo akihudhuria atajionea maendeleo yake. “Nitapenda sana iwapo rais Mwinyi atahudhuria siku ya Tamasha ili aweze kushuhudia muendelezo wa Tamasha tangu alipolizindua mwaka 2000,” alisema Msama. Alisema hadi sasa maandalizi yamekamilika hivyo mashabiki wa nyimbo za injili wakae mkao wa kula wakisubiria tamasha hilo mapema mwanzoni mwa mwezi ujao. “Mashabiki wakae tayari maandalizi yamekamilika, tunachosubiri ni siku yenyewe ifike, waimbaji maarufu watakuwepo wakisufu na kuabudu, hivyo ni wakati wenu mzuri wa kwenda ku...