WAZIRI MKUU KUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI JAPAN

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,Machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa.
Waziri Mkuu, MizengoPinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Japan, Bw. Masahito Kawashima kabla ya kuzungumza na ujumbe wa wawekezaji wa Kijapan kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo Machi 17, 2015.
Waziri Mkuu, MizengoPinda akisalimian na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Japan, Bw. Masahito Kawashima kabla ya kuzungumza na ujumbe wa wawekezaji wa Kijapan kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo Machi 17, 2015. Katikati ni Ofisa wa Ubalozi wa tanzania nchini Japan , Francis Mosongo.

Waziri mkuu, Mizengo Pinda na mkewe wakitia saini kitabu cha wageni kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo nchini Japan baada ya kuwasili ubalozini hapo kuzungumza na Watanzania waishio Japan Machi 17, 2015. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza muda wake, Salome Sijaona na Wapili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Batilda Buriani na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mahadh Maalim.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watoto, Neema Mosongo ( kulia) na Stacey Kambona baada ya kuwasili kwenye ubalozi wa Tanzanianchini Japanuliopo Tokyo kuzungumza na watanzania waishio nchini humo Machi 17, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watoto, Petro Mosongo (kulia), Neema Mosongo (wapili kulia) na Stacey Kambona baada ya kuwasili kwenye ubalozi wa Tanzania jijini Tokyo kuzungumza na watanzania waishio Japan Machi 17, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waoishi nchini Japan.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB