Posts

Showing posts from July 14, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA JAJI MSTAAFU, BUXTON CHIPETA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, aliyefariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Makamu alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini leo Julai 19, 2013.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar.    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa ndugu wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo, nyumbani kwa marehemu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia ...

President Kikwete meets Standard Chartered CEO Liz Lloyd at Dar es Salaam State House

Image
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Standard Chartered Bank Chief executive Officer(CEO) Liz Lloyd at Dar es Salaam State House yesterday afternoon. On the left is Head of Corporate Affairs Ms.Juanita Mramba. President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pose for a photograph with the Standard Chartered Bank Chief Executive Officer(CEO) Liz Lloyd(left) at State House Dar es Salaam yesterday afternoon. On the right is the bank’s Head of Corporate Affairs Ms. Juanita Mramba (photos by Freddy Maro)

Balozi Mulamula awasilisha hati za utambulisho kwa Rais Obama Ikulu ya Marekani

Image
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula akiwa na Rais Barack Obama mara baada ya kuwasilisha hati ya utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama White House jijini Washington DC Picha na Michuzi Blog

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UKIMWI LA KIMATAIFA ABUJA NIGERIA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe, wakati walipokutana katika Mkutano wa 12 wa Afrika  unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na  Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za  Afrika.Picha na OMR  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Shirika  la Umoja wa Mataifa la Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe, baada ya mazungumzo yao walipokutana katika Mkutano wa 12 wa  Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa  na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za  Afrika.Picha na OMR...

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB

Image
                  Rais Dkt.Jakaya  Mrisho Kikwete akizindua mpango wa huduma ya Benki ya Posta Tanzania(Tanzania Postal Bank),TPB Popote katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Profesa  Leticia Rutashobya, Waziri wa Fedha Dr.william Mgimwa, Naibu Waziri wa  Fedha  Bi.Saada Mkuya(wanne kushoto) na kulia ni mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo bwana Moshingi  Sabasaba. Huduma hiyo ina lengo la kusambaza huduma za kibenki kwa wananchi waishio mbali hususan vitongojini na  sehemu za vijijini (picha na Freddy Maro).   Rais Kikwete akipewa maelezo mafupi namna ya kuitumia huduma hiyo ya  TPB POPOTE kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Posta.     Mgeni rasmi,Rais Kikwete akikabidhiwa zawadi kut0ka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya  ...

HASHEEM THABEET NDANI YA UWANJA WA TAIFA KWENYE MECHI YA TAIFA STARS vs UGANDA

Image
Mtanzania anayecheza kikapu katika Ligi ya Marekani maarufu kama NBA, Hasheem Thabeet, amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka kwenye Uwanja wa Taifa,Dar. Thabeet anayecheza katika timu ya Thunder, aliibuka na kuwasalimia mashabiki wakati Taifa Stars ikivaa Uganda nao walimshangilia kwa nguvu sana.