RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB

8E9U0880                 Rais Dkt.Jakaya  Mrisho Kikwete akizindua mpango wa huduma ya Benki ya Posta Tanzania(Tanzania Postal Bank),TPB Popote katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Profesa  Leticia Rutashobya, Waziri wa Fedha Dr.william Mgimwa, Naibu Waziri wa  Fedha  Bi.Saada Mkuya(wanne kushoto) na kulia ni mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo bwana Moshingi  Sabasaba. Huduma hiyo ina lengo la kusambaza huduma za kibenki kwa wananchi waishio mbali hususan vitongojini na  sehemu za vijijini
(picha na Freddy Maro).


 Rais Kikwete akipewa maelezo mafupi namna ya kuitumia huduma hiyo ya TPB POPOTE kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Posta.
  Mgeni rasmi,Rais Kikwete akikabidhiwa zawadi kut0ka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya