M-PESA YAZINDULIWA NDANI YA UCHUMI SUPERMARKET
Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Lenana (kushoto) na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh wakikata utepe kuzindua rasmi duka la Vodacom ndani ya Uchumi Supermarket ikiwa ni huduma ya kwanza na ya kipekee nchini. Duka hilo linawawezesha wateja wa Vodacom kupata huduma za kampuni ikiwemo moderm, vocha, usajili wa nambari zao, M-pesa n.k wanapofika kwenye Supermarket hiyo kwa ajili ya kupata kufanya manunuzi ya mahitaji mengine. Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh akiongea na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa duka la Vodacom ndani ya Supermarket ya Uchumi. Vodacom imezindua pia huduma za malipo kwa M-pesa kwa wateja wanaofanya manunuzi ndani ya Supermarket hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh akitumia huduma ya M-pesa kulipia bidhaa alizonunua ndani ya Supermarket ya Uchumi ya jijini Dar es sa...