Posts

Showing posts from September 22, 2013

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA GYKRUM,ARUSHA

Image
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), Bi. Ruth Koya akisoma hotuba fupi mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akifungua rasmi jiwe la msingi katika mradi wa maji wa kijiji cha Gykrum, Karatu Mjini, mkoani Arusha. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akipata maelekezo kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), Bi. Ruth Koya pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge, katikati ni Mama Tunu Pinda. Picha zote na Michuzi Blog

MKUTANO WA DR SLAA WASHINGTON DC WAFANA

Image
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa Jumapili Sept 22, 2013 aliongea na Watanzania wa DMV na vitongoji vyake kuhusu mstakabali mzima wa Tanzania, kisiasa, kiuchumi na huku akigusia mali asili na utalii, kusafirishwa kwa wanyama nje ya nchi kinyemela.  Mwenyekiti wa CHADEMA DMV, Bwn. Kalley Pandukizi akizungumuza na kueleza historia ya tawi la CHADEMA DMV lilivyoanzishwa kabla ya kumkaribisha katibu wa tawi DMV, Bwn. Liberatus Mwang'ombe.  Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na Katibu wa CHADEMA DMV Bwn. Liberatus Mwang'ombe. Bi. Josephine Mshumbuzi akiongea na wanaDMV kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere. Mama Leticia Nyerere akipeana Mkono na Mchungaji Materu katika Mkutano wa Chadema DMV uliohutubiwa na Dr Slaa Pichani ni baadhi ya Wakazi wa Washington DC (DMV) Waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa.

ZIARA YA MHE. HARRISON MWAKYEMBE NCHINI MAREKANI

Image
Mhe. Harrison Mwakyembe alipotembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tanzania House, Washington DC. Katikati ni Mhe. Waziri Harrison Mwakyembe akiwa na ujumbe wake akiwa na baadhi ya maofisa wa Ubalozi huo Bw. Paul Mwafongo (wa tatu Kushoto) na Bw.Suleiman Saleh (wa tatu kulia). Mhe. Harrison Mwakyembe(Mb.)Waziri wa Uchukuzi akipokewa na mwenyeji wake Bw.Robert Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Michigan mara baada ya kuwasili hotelini alikofikia. Mhe.Waziri Mwakyembe katika picha ya pamoja na Bw. Shumake na Bw. Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC. Juu na chini ni Mhe. Mwakyembe katika taswira mbali mbali na Bw. Joelson, Mmiliki wa kituo cha kufundisha Urubani cha DCT katika ziara yake kituoni hapo ambapo alionyeshwa ndege za aina mbali mbali pamoja na kupata historia ya kituo hicho. Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) na Ujumbe wake Bw. Peter Lupatu , Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri,Wizara ya Uchukuzi, B