Lema aipeleka CHADEMA London
ALIYEKUWA Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amepeleka harakati za Movement For Change zinazoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nchini Uingereza. Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka London Uingereza, Lema alisema kuwa moja ya shughuli atakazofanya akiwa huko ni kufungua matawi ya CHADEMA. “Nilipofika tu Watanzania wengi wanaoishi hapa walionyesha nia ya kutaka kuwa na tawi katika jiji la London na tutakuwa na mikutano kadhaa ya ndani ya kubadilishana mawazo,” alisema Lema. Lema ambaye amepata kuwa mbunge machachari ndani ya Bunge la Muungano, alisema CHADEMA itatumia nafasi hiyo kupata mawazo ya Watanzania wanaoishi nje ambao mara nyingi hawakuwa na fursa ya kutoa mawazo yao. “Ingawa nimekuja kwa shughuli binafsi, nitatumia nafasi hiyo kueneza harakati zetu za Movement For Change na kubwa zaidi kupata maoni na michango ya mawazo ya Watanzania wanapenda mabadiliko nchini,” alisema Lema. Tangu alipovuliwa ubunge na Mahakama, Lema ame...