Dr. Slaa Receives A State Reception In Alabama Capitol
Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willibrod Slaa katika ziara yake nchini Marekani iliyoandaliwa na umoja wa vyuo vikubwa nchini humo ya kujifunza mambo mbali mbali, imemfikisha leo katika jimbo la Alabama na kupokelewa na wakuu wa jimbo hilo akiwemo Gavana pamoja na Waziri wa biashara. Alabama ni moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo siku za nyuma. Uchumi wake ulitegemea kilimo kwa 90%. Miaka 25 iliyopita, viongozi wake walibuni mikakatati ya kulibadilisha. Leo, Jimbo la Alabama ndio moja ya majimbo yenye viwanda vikubwa vya magari kama Honda, Mercedes Benz, Airbus, Hyundai, Raytheon, Space station, Wallgreens na mengineyo Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa. Kupitia kauli mbiu yake ya “Vision Tanzania” Dr. Slaa alipata kukutana na viongozi wa jimbo hilo ili aweze kujifunza mbinu ambayo ataweza kuwarudishia watanzania ili nao waondokane na umasikini. Licha ya yote, Gavana wa jimbo hilo pamoja na mawaziri wake, wako tayari kushirikiana na Tanzania kwe...