Posts

Showing posts from January 19, 2014

Uzinduzi wa Operesheni ‘M4C Pamoja Daima’ Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa Wazindua Songea,Namtumbo,Mbinga na Mbunge wa Ubungo John Mnyika Azindua Uyui,Tabora Kwa Kutumia Usafiri wa Helikopta Tatu

Image
 Mbunge wa Iringa Mjini Mh Peter Msigwa akiwa mbele ya Moja ya Chopa wanayotumia katika Operesheni Pamoja Daima  Mwenyekiti wa chadema na mbunge wa hai freeman mbowe akiwasili,nyuma yake ni mbunge wa singida magahribi tundu lissu  Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akiwasili Songea kwa helikopta(haipo pichani)nakupokelewa kwa shangwe.  Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Songea.  Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Namtumbo.  Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Mbinga  Mbunge wa iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwahutubia wakazi wa Songea. Mbunge wa Iringa Mjini Mh Peter Msigwa akiwahutubia wakazi wa Mbinga.  Mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika akiwahutubia wakazi wa Uyui, Tabora katika uzinduzi wa Operesheni Pamoja Daima Wakazi wa Uyui waliohudhuria katika uzinduzi wa Operesheni Pamoja Daima jana .Picha Zote na Chadema

WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE ATEMBELEA CLOUDS MEDIA GROUP LEO

Image
 Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipowasili mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar,pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kwenye moja ya Ofisi za kampuni hiyo,alipofanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo  na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.  Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akitoa ufafanuzi mfupi  kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipotembelea kitengo hicho cha habari na kujionea uandaaji wa habari ya televisheni na redio unavyofanyika.  Mmoja wa Watangazaji kipindii cha Mic

PICHA: KIPINDI CHA THE MBONI SHOW CHAWAALIKA WASANII WA FILAMU NCHINI STEVE NYERERE NA ELIZABETH MICHAEL "LULU" WALIO CHINI YA KAMPUNI YA PROIN PROMOTIONS LIMITED

Image
 Msanii wa Maigizo Tanzania Steve Mongere aka Steve Nyerere akisalimiana na Mwendesha Kipindi cha The Mboni Show , Mboni Masimba (Wa Kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili ndani ya mjengo ambapo kipindi hiko hurekodiwa Pembeni ni Msanii nguli wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael "Lulu" akifuatiwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa Filamu za Kitanzania Nchini. Msanii Nguli na mahiri aliye chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited Elizabeth Michael "Lulu" akisikiliza kwa makini wakati msanii mwenzie Steve Nyerere alipokuwa akiongea katika kipindi cha The Mboni Show  Mwendeshaji wa Kipindi cha The Mboni Show Mboni Masimba (Wa Kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Muigiza Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu aliye chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited mara baada ya kipindi kumalizika  Meneja masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Ev

MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA MZEE MAKAMBA

Image
Mzee Yusufu Makamba akishauriana jambo na mwanae January Makamba wakati wa shughuli za mazishi zikiendelea. Mzee Yusufu Makamba amefiwa na mama yake mzazi aliyefahamika kama Mariam Masau Kivugo  kilichotokea  Marehemu Mariam Masau Kivugo amezikwa katika kijiji cha  Mehazangulu mkoani Tanga  tarehe 21 January 2014. Mzee Yusufu Makamba akiwa na mwanae January Makamba wakitafakari jambo baada ya kupata msiba mkubwa  wa kufiwa na Mama mzazi wa Mzee Yusufu Makamba, Mariam Kivugo. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Majura Bulembo akitoa salaam za pole kwa wafiwa wakati wa mazishi ya Bibi Mariam Masau Kivugo. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa salaam za pole kwa niaba ya Chama  kwa Mzee Yusufu Makamba na Familia yake wakati wa mazishi ya Mama wa Mzee Yusufu Makamba. Mamia ya watu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba wakati akitoa salaama za shukrani kwa niaba ya familia kwa wananchi wote waliojitokeza

CUF WAZINDUA KAMPENI ZA JIMBO LA KIEMBE SAMAKI

Image
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho Professa Ibrahim Haruna Lipumba katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki  katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba na viongozi wengine wa chama hicho wakirusha maputo kama ishara ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba akimnadi mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, Abdulmalik Haji Jecha, katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI MPANGO MPYA WA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

Image
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na watoto waliozaliwa kutoka katika familia zinazoishi na virusi vya ukimwi lakini zimeweza kupata watoto ambao ni salama baada ya kutumia dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Wazazi wa watoto hao walitoa ushuhuda wao wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto  (PMTCT OPTION B+) kwa mkoa wa Dar es Salaam zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere tarehe 22.1.2014.PICHA NA JOHN  LUKUWI.  Washiriki waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza na kushangilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete