MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI MPANGO MPYA WA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

IMG_3852Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na watoto waliozaliwa kutoka katika familia zinazoishi na virusi vya ukimwi lakini zimeweza kupata watoto ambao ni salama baada ya kutumia dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Wazazi wa watoto hao walitoa ushuhuda wao wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto  (PMTCT OPTION B+) kwa mkoa wa Dar es Salaam zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere tarehe 22.1.2014.PICHA NA JOHN  LUKUWI. IMG_3923Washiriki waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza na kushangilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.
IMG_3946Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono  washiriki waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa huduma mpya za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.

IMG_3950Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, (PMTCT OPTION B+) kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.IMG_4031Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia wazazi wa mtoto Debora Andrew (aliyembeba) , mwenye umri wa miezi 9, ambaye hana maambukizi ya VVU kutoka kwa wazazi wake wanaoishi na virusi vya ukimwi ambao hutumia dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Mama Salma alikutana na wanafamilia hao wakati wa uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi kwa Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB