Posts

Showing posts from May 12, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA DIRECT AID CHARITY ORGANISATION YA KUWAIT

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Dkt.Abdul RahmanAl Muhailan ambaye ni mwenyekiti wa asasi ya Direct AID Charity Organisation leo (picha na Freddy Maro)

Zitto: Pendekezo binafsi kuzuia unyonyaji dhidi ya Wasanii wa Tanzania katika Biashara ya Miito

Image
PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES) Kwenda kwa : DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara  Kuhusu : BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES) Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara. USIRI Biashara hii ya “Ring Back Tones” (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao nao huingia mikataba na Wasanii (Content Creators). Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchi

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO

Image
MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) leo katika ukumbi wa White House mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na wengine kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu imemteua mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chambani, Pemba Mattr Said . (Picha na Bashir Nkoromo)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Amtembelea Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa Nchini Tanzania Francisco Montecillo Padilla na kumpa pole

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Mhe. Francisco Montecillo Padilla, Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa hapa nchini mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kumpa pole kufuatia shambulio la bomu  lililotokea Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013  na kupelekea watu watatu kufariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa. Balozi Padilla alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa  katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jimbo Kuu la Arusha wakati tukio hilo linatokea. Mhe. Balozi Padilla akiwa katika  mazungumzo na Mhe. Membe kuhusu tukio hilo  ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa anaamini suala hilo litapita na wahusika kupatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria. Mhe. Membe akiagana na Mhe. Balozi Padilla mara baada ya kuzungumza naye.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Viongozi wanapogongana Ziarani - Mbowe na Ole Medeye Uso kwa Uso Bomang’ombe

Image
M wenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye. Viongozi hao walikutana juzi eneo la Bomang'ombe, wilayani Hai, kila mtu akiwa katika ziara yake. Wakati Mbowe alikuwa anaendelea na ziara ya kuzungukia wananchi katika vijiji mbalimbali jimboni kwake Hai, Medeye alikuwa katika ziara yake binafsi maeneo ya jimbo hilo. Ziara ya Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai katika picha, akikagua ujenzi na uhai wa chama (Chadema) ngazi ya misingi/vitongoji ambapo anakutana na kuzungumza na viongozi wa misingi hiyo. Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Hai, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa chama hicho Kijiji cha Mtakuja, Mzee Ally Mbatia. Mbowe yuko katika ziara ya kukagua uhai na kuimarisha ujenzi wa chama katika ngazi ya chini kabisa ya chama hicho, msingi, kwenye maeneo ya vitongoji mbalimbali ka