TUKIO KATIKA PICHA: MASHABIKI WA SIMBA WAFANYA FUJO UWANJA WA TAIFA BAADA YA REFA KUTOA PENATI DAKIKA YA 90
Askari wa kutuliza ghasia, FFU, wakipiga mabomu ya machozi hewani kuwatawanya mashabiki wa Simba, waliokuwa wakifanya fujo kwa kung'oa viti na kurusha uwanjani baada ya timu ya Kagera Sugar, kusawazisha bao lao kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 90+, iliyotolewa na mwamuzi, Mohamed Theophile. Penati hiyo imepatikana baada ya beki wa Simba Joseph Owini, kumchezea vibaya Daud Jumanne, penati hiyo iliyopigwa na Salum Kanon, imezifanya timu hizo kutoka sare ya 1-1, wakati bao la SImba likifungwa na Amis Tambwe katika dakika ya 45. Askari wakimdhibiti mmoja wa mashabiki wa Simba. **************************************** BAO la beki wa kulia wa Kagera Sugar, Salum Kanoni lilipoteza amani ndani ya Uwanja wa Taifa baada ya mashabiki wa Simba kuanza kung’oa viti hali iliyosababiosha Polisi walipue mabomu ya machozi kutuliza vurugu hizo. Kagera ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Amisi Tambwe katika kipindi cha kwanza, walipata bao la kusaweazisha kupitia kwa