Posts

Showing posts from May 26, 2013

RAIS DKT. SHEIN ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA KIHISTORIA YA DR.SUN YAT-SEN’S KATKA MJI WA NANJING CHINA

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakisalimiana Waongoza Wahusika wa FAya Dr.Sun Yat-sen’walipofika na ujumbe wake kupata historia ya makumbusho hayo huko Nje ya Mji wa Nanjing,katika Jimbi la Jiangsu nchini China,wakiwa katika ziara ya Kiserikali jana. [Picha na Ramadhan Othman,Nanjing China.] RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiuliza jambo akiwa na Ujumbe wake wakati walipotembelea    Makumbusho ya Kihistoria ya Dr.Sun Yat-sen’s yaliyopo   Nje ya Mji wa Nanjing,katika Jimbo la Jiangsu nchini China,wakiwa katika ziara ya Kiserikali jana. [Picha na Ramadhan Othman,Nanjing China.] Baadhi ya Wananchi wa Mitaa mbali mbali katika mji wa Nanjing hufika kutembelea sehemu ya Makumbusho ya  kihistoria pamoja na Watalii kutoka nje ya mji huo,kuangalia mandhari yakupendeza na  kupanda mlima wa kihistoria wa Dr,Sua Yat-sen’s,katika Jimbo la Jiangsu.{Picha na Ramadhan Othman,Nanj

MAKAMU WA RAIS DKT.BILAL ATEMBELEA CHUO KIPYA CHA TEHAMA CHA VETA KIPAWA JIJINI DAR

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza na kumtazama Mwanafunzi wa  umeme, Elia Michael, alipokuwa akielezea jinsi wanafunzi hao wanavyoweza kuunda Sacket ya umeme inayoweza kuongoza mashine mbalimbali za  umeme, wakati Makamu alipotembelea katika Chuo kipya cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2013. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza na kumtazama Mwanafunzi wa  umeme, Elia Michael, alipokuwa akielezea jinsi wanafunzi hao wanavyoweza kuunda Sacket ya umeme inayoweza kuongoza mashine mbalimbali za  umeme, wakati Makamu alipotembelea katika Chuo kipya cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2013. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbi kumbu mbele ya jengo  la Chuo cha VETA, wakati alipotembelea chuo hicho cha Tehama cha VETA Kipawa, leo Juni 1, 2013

WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA AKIWA MKOANI RUKWA SIKU YA MAZINGIRA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiteta na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Seif Rashidi  (kushoto) na askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Sumbawanga, Damiano Kyaruzi  baada ya kuweka jiwe la Msinhgi  Taasisi ya Mafunzo ya Afya ya Mtakatifu Bakhita ya Namanyere Rukwa  ikiwa ni moja ya shuguli alizofanya kama mgeni wa siku ya Mangira Duniani iliyofanyika kitaifa, Namanyere Juni 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe fupi ya uwekaji jiwe la msingi la Taasisi ya Mafunzo ya Afya ya Mtakatifu Bakhita ya Mjini Namanyere ikiwa ni moja ya shughuli za siku ya mazingira duniani iliyofanyika kitaifa, mjini Namanyere juni 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DORIS MOLEL NDIYE REDD'S MISS TABATA 2013

Image
Redd's Miss Tabata 2013,Doris Molel akipunga mkono kwa mashabiki wake muda mfupi baada ya kutawazwa rasmi kuwa Mrembo wa Kitongoji cha Tabata,Shindano hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Da'west Park,Tabata jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jumamosi.Wengine pichani ni Mshindi wa Pili wa shindano hilo,Upendo Lema (kulia) pamoja na Mshindi wa Tatu,Rachel Mushi. Redd's Miss Tabata aliemaliza muda wake,Noella Michael (alieketi) akisuburi kutangazwa kwa mrithi wake. Warembo walioingia hatua ya tano bora katika Shindano la Redd's Miss Tabata 2013. Kumi Bora. Warembo wa Tabata wakionyesha shoo yao ya ufunguzi.

MWANA FA AWA BALOZI WA SAMSUNG TANZANIA

Image
Msanii maarufu wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva’ Hamisi Mwijuma ‘Mwana FA’ (kulia) akiwa ameshikilia simu ya kiganjani aina ya Samsung Galax 4 aliyokabidhiwa muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa Balozi wa Samsung Galax 4.  Msanii maarufu wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva’ Hamisi Mwijuma ‘Mwana FA’ (kulia) akiwa ameshikilia simu ya kiganjani aina ya Samsung Galax 4 aliyokabidhiwa na Meneja wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar jijini Dar es Salaam leo wakati kampuni hiyo ikimtangaza kuwa Balozi wa wa Simu hiyo nchini.   Msanii maarufu wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva’ Hamisi Mwijuma ‘Mwana FA’ (wa tatu kushoto) akiwa ameshikilia simu ya kiganjani aina ya Samsung Galax 4 aliyokabidhiwa na Meneja wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar (watatu kulia)  jijini Dar es Salaam leo wakati kampuni hiyo ikimtangaza kuwa Balozi wa wa Simu hiyo nchini. Wengine pichani ni Mamodel wa Samsung (kulia na kushoto), Mkuu wa Biashara kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Manoj Changara

WAZIRI NCHIMBI AKUTANA NA UJUMBE WA EU KUZUNGUMZIA HALI YA ULINZI NA USALAMA

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi katika Kikao na Wawakilishi wa Nchi za Umoja wa Ulaya waliotembelea Wizarani jana.  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.  (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi). TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Serikali  ya Tanzania  imesema itahakikisha inaendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa watanzania na raia wa kigeni waliopo na wanaoendelea kutembelea hapa nchini  kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za binafsi na kimaendeleo  ili watu wote  waweze kutekeleza majukumu yao na  kuishi kwa amani na usalama hapa nchini.  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema hayo leo wakati akizungumza katika kikao baina yake na Ujumbe wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya na mabalozi wa  nchi hizo hapa nchini kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo. Mabalozi hao ni Dk. Ad Koekkoek wa Uholanzi, Marcel Escure wa Ufaransa,  Diana Melrose wa Uingerez

MHESHIMIWA FREEMAN MBOWE AKIHUTUBIA WAKAZI WA SONGEA

Image

Godbless Lema - MESEJI YA VITISHO ILITOKA KWA MKUU WA MKOA

Image
Tarehe 21 /5/2013 Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) L iberatus Sabas ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliongea na waandishi wa habari juu ya shutuma zangu juu ya ujumbe wa maneno mfupi niliopokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Magessa Mulongo siku ya tarehe 25.04.2013 kutoka kwenye namba anayotumia mkuu wa Mkoa namba 0752960276 namba ambayo imesajiliwa kwa jina la Magessa Mulongo kwenda namba 0764150747 namba ambayo imesajiliwa kwa jina la Neema Lema namba ninayo tumia Mimi , ujumbe unaosema  “ Umeruka kihunzi cha kwanza nitakuonyesha kuwa mimi ni Serikali , ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi “ Nimesikitishwa na kufedheheshwa sana na taarifa hii ambayo sasa inathibitisha bila mashaka kuwa Jeshi la Polisi Arusha hasa Mkuu wake anatumika na sina shaka kusema kuwa yeye ni KIPEPERUSHI cha Mkuu wa Mkoa , baada ya Mimi kupokea ujumbe huu tarehe 25/4/2013 nilitoa taarifa kwa vyombo vya habari na nia yangu ya kwenda mahakamani juu ya vitisho hivi . H

RAIS DKT. KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI ADDIS ABABA, ETHIOPIA

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Mohamed Morsi walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Mohamed Morsi walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR)  professor Ntumba Luaba  na ujumbe wake   walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya  mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamaica Bi.  Portia Simpson Miller   walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya  mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika

KINANA, NAPE WATUA IRINGA

Image
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakisalimia baadhi ya viongozi, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Iringa asubuhi hii, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba, mkoani Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu.  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa na viongozi wa mkoa wa Iringa. Nyuma ni Nape Nape naye akiwa na wenyeji.  Kinana akisaini kitabu cha wageni Uwanja wa Ndege wa Iringa baada ya kuwasili uwanjani hapo asubuhi hii. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msavatavangu Nape akisaini kitabu cha wageni.

RAIS WA ZANZIBAR AMTEMBELEA SHEHA ALIYEMWAGIWA TINDIKALI

Image
        Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein akimuangalia Sheha wa Shehia ya Tomodo wilaya ya Magharibi Unguja, Mohammed Said Kidevu (kulia) jinsi alivyoathirika na tindikali aliyomwagiwa na mtu asiyefahamika. Bw. Kidevu alimwagiwa tindikali hiyo juzi alipokuwa akirudi nyumbani kwake kutoka kuchota maji; amelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar. Kushoto ni Dkt. Salim Mohammed.             Bw. Mohammed Kidevu, Sheha wa Shehia ya Tomondo, Zanzibar (kulia) akimuelezea Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein jinsi alivyomwagiwa tindikali hiyo. Bw. Kidevu alimwagiwa tindikali hiyo juzi na mtu asiyefahamika akielekea nyumbani kwake akitoka kuchota maji. Wa pili kulia ni kaka wa Bw. Kidevu, Sudu Mgeni Said.

MARTHA GEWE ANYAKUA TAJI LA REDD'S MISS UKONGA 2013

Image
  Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Ukonga 2013, Martha Gewe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Diana Joachim (kushoto) pamoja na mrembo aliyeshika nafasi ya tatu, Natasha Mohamed mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa ndio washindi wa shindano hilo Usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam. Martha aliwashinda warembo wengine 12 katika shindano hilo. Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Ukonga 2013 wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni Vanesa Magile, Matha Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed na Nancy Abasy shindano lilifanyika Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam. Martha.   Baadhi ya washiriki wa Shindano la Redd’s Miss Ukonga 2013 wakicheza show ya ufunguzi wa shindano lao lililofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Wenge Garden Ukonga jijini Dar es Salaam.   Baadhi ya majaji wa shindano hilo wakiongo