Waziri Muhongo akataa chakula hotelini aenda kwa mamalishe
Profesa Muhongo WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa chakula Hoteli ya Mount Meru na kwenda kula chakula cha Mamalishe. Tukio hilo lililowashangaza watu 13 waliokuwa katika msafara wake lilitokea hivi karibu wakati Profesa Muhongo alipokwenda Arusha kwenye mkutano wa wataalamu wa umeme wa nchi 11 za Afrika Mashariki, Kati na Kaskazini. Waziri Muhongo aliandaliwa chakula hotelini hapo, lakini aliwashangaza wenyeji wake ambao ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na uongozi wa wizara yake. Baada ya kufika katika mgahawa wa Pizza Point uliopo katikati ya mji wa Arusha, Waziri Muhongo aliagiza ugali na samaki kwa bei ya Sh7,000. Tukio la waziri huyo kukataa kula chakula cha usiku katika hoteli hiyo ya kifahari, iliwashangaza hata wafanyakazi wa mgahawa huo baada ya kupata taarifa hiyo. Ingawa haikufahamika mara moja sababu za waziri huyo kukataa kula katika hoteli hiyo kutokana na kuchukua uamuzi ghafla, lakini taarifa za ndani zinadai haku...