Posts

Showing posts from March 17, 2013

RAIS KIKWETE AZINDUA UWANJA WA AZAM COMPLEX MBAGALA

Image
Rais Jakaya Kikwete akifunia kitambaa kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Soka wa Azam Complex, unaomilikiwa na timu ya Soka ya Azam Fc, uliopo Mbagala Chamazi jijini Dar es Salaam leo. Rais Jakaya Kikwete akikata utepe,wakati wa uzinduzi rasmi wa uwanja wa huo. Rais Jakaya na ujumbe wake wakitembelea sehemu za uwanja huo, hawa wakipita karibu na Bwawa la kuogelea lililopo ndani ya uwanja huo. Picha na Habari Mseto

Rais Kikwete amtembelea Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hospitali ya Taifa Muhimbili

Image
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyepumzishwa katika chumba cha Dharura katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.Mzee Kingunge alikimbizwa Hospitalini Hapo Baada ya Kujisikia Vibaya.jopo la Madaktari Bingwa linamfanyia uchunguzi Mzee Kingunga ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.Aliyesimama Nyuma ya Rais ni mke wa Mzee Kingunge na kushoto ni Mtoto wa Mzee Kingunge Bwana Kinjekitile.(picha na freddy Maro)

WAKAZI WA ARUSHA WAPOKEA KWA FURAHA UJIO WA TUSKER LITE

Image
Meneja wa bia ya Tusker Lite Bi. Anitha Msangi kielezea wadau jinsi bia ya Tusker Lite ilivyotengenezwa kwa vimelea asili na yenye wanga kidogo sana katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi. Wadau wa bia ya Tusker Lite na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakionyesha furaha na kuipokea bia ya Tusker Lite a kugonganisha chupa kwjijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi. Nakaaya Sumari akifurahia jambo na MC katika hafla hiyo. Mama akifurahia zawadi ya glass za Tusker Lite baada ya kuibuka mshindi wa kucheza muziki katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya...

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUMU TOKA KWA RAIS WA BOTSWANA

Image
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Botswana uliowasilishwa na  Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mhe Pandu Skelemi jana leo Ikulu jijini Dar es salaam.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Botswana uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mhe Pandu Skelemi jana Ikulu jijini Dar es salaam.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Botwana Mhe Pandu Skelemi baada ya kupokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa nchi hiyo jana Ikulu jijini Dar es salaam.  PICHA NA IKULU

LADY JAYDEE AZINDUA VIDEO YA “JOTO HASIRA” NYUMBANI LOUNGE

Image
Lady JayDee akiimba kwa kushirikiana na waimbaji wa bendi ya  Machozi bendi anayoimiliki mwenyewe wakati wa onesho hilo. Jaydee akiwa kando ya gari lake mara baada ya kuwasili Nyumbani Lounge tayari kwaajili ya uzinduzi wa Video yake mpya ya Joto Hasira. Mashabiki wa mwanamuziki huyo wakicheza stejini  huku wakiwa wamepanga mstari  Dida Wa Mchops akiongoza mashabiki wa mwanamuziki Lady JayDee wakati wakicheza stejini Mbunifu wa Mavazi Asia Idarous akipozi kwa picha na Mdau Bhoke wakati wa onesho hilo. Mboni Masimba katikati akiwa katika picha ya pamoja na Juma Pinto na Mdau Fred Maeda Mamaa Shamimu wa 8020fashionblog akiwajibika kwa kupata taswira za onesho hilo. Mdau Bhoke akipozi kwa picha Mdau Jane na mdogo wake nao walijitokeza katika uzinduzi huo wa video ya Joto Hasira. kutoka kulia ni Monica na kutoka kushoto ni Mboni Masimba na Shamimu Mwasha Juma Pinto kulia  na wadau mbalimbali wakishoo Love kwa picha

UZINDUZI WA SHINDANO LA REDD’S MISS TANZANIA 2013

Image
Baadhi ya Warembo walioshirikishi Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 wakicheza muziki wa aina ya Kwaito wakjati wa tafrija maalum ya uzinduzi wa Mashindano ya Miss Tanzania 2013 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Machi 14, 2013. Kulia ni Redd’s Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred.  Redd's Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred (katikati) akigonganisha glass na Mkurugeni wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni Wadhamini wakuu wa Shindano la Miss Tanzania,Kushilla Thomas (klia) pamoja na Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko Hashim Lundenga ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party),iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ya Jijini Dar es Salaam, ambao ndio waandaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akitoa...

TAARIFA YA RIDHIWANI KIKWETE KUKANUSHA YALIYOANDIKWA DHIDI YAKE KATIKA MITANDAO YA JAMII

Image
Ridhiwani Kikwete Ndugu zangu, habari za mapumziko ya mwisho wa wiki. Yapo mambo machache ningependa kuwashirikisha ili kuweka kumbukumbu sawa, na pia kuzuia upotoshaji ambao unaweza kujitokeza siku za usoni iwe kwangu, kwako au kwa mtu mwingine. Mojawapo ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza siku za karibuni hasa katika suala la Teknolojia na habari ni jambo la sheria za faragha (privacy and privacy laws). Tumeshu hudia kufungwa kwa gazeti za News of The World mali ya bilionea Rupert Murdoch wa Kimarekani baada ya kudhihirika alitumia wataalam wa teknolojia (hackers) kutafuta siri za watu mashuhuri kwa kuingia katika simu zao za mkononi kinyume cha utaratibu na sheria za faragha (Privacy Laws). Tumeshuhudia pia wahalifu hao hao wa mtandao wakifanya mengi kama kuvamia kwa mitandao ya makampuni makubwa kama Sony na mengineyo na hata katika mitandao hii ya kijamii upo wakati marafiki zako wanakwambia mbona umenitumia kitu kisichoeleweka, na baadaye kuja kugundua kwamba si wewe uliyefa...