Maalim Seif awasili jijini London
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, akiweka saini kwenye Kitabu cha Wageni kwenye Ofisi wa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi hizo za Ubalozi. Pichani: Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, akishuhudia uwekaji wa saini, mara baada ya kumkaribisha Ofisini hapo. Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa. Peter Kallaghe, wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi, Wajumbe na Wawakilishi kutoka Serikali ya Zanzibar Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliwasili London, Uingereza juzi usiku (Jumanne, 11 Septemba 2012) kwa ziara ya siku nne akitokea Marekani alikokwenda kuhudhuria Mkutano wa Democratic Party, kwa mwaliko rasmi wa chama hicho. Maalim Seif jana (Jumatano, 12 Septemba 2012) alitembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo hapa London na kuzungumza na Maafisa wa Ubalozi huo na baadae kula nao c...