Maalim Seif awasili jijini London



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, akiweka saini kwenye Kitabu cha Wageni kwenye Ofisi wa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi hizo za Ubalozi. Pichani: Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, akishuhudia uwekaji wa saini, mara baada ya kumkaribisha Ofisini hapo.
Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa. Peter Kallaghe, wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi, Wajumbe na Wawakilishi kutoka Serikali ya Zanzibar


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliwasili London, Uingereza juzi usiku (Jumanne, 11 Septemba 2012) kwa ziara ya siku nne akitokea Marekani alikokwenda kuhudhuria Mkutano wa Democratic Party, kwa mwaliko rasmi wa chama hicho. Maalim Seif jana (Jumatano, 12 Septemba 2012) alitembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo hapa London na kuzungumza na Maafisa wa Ubalozi huo na baadae kula nao chakula cha mchana. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar leo asubuhi amekutana na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Uingereza, Mheshimiwa Mark Simmonds na mchana huu anakutana na mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki waliopo hapa London. Kesho Mheshimiwa Maalim Seif anatarajiwa kukutana na Watanzania wote walioko London katika sehemu itakayotangazwa hapo baadae, kabla ya kuanza safari ya kurejea Tanzania Jumamosi asubuhi.

Picha na habariMr. A. Rashid Dilunga
ICT - Manager
Tanzania High Commission
Tanzania Trade Centre
3 Stratford Place
London W1C 1AS
Tel: +44(0) 207 758 8070
Fax: +44(0) 207 758 8073
Email: dilunga@tanzatrade.co.uk
Web: tanzatrade.co.uk


williammalecela.blogspot.com

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB