TANZANIA TOURIST BOARD 2013 AWARDS PRESENTATION
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba akiongea machache kuwashukuru Mbalozi wa wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumatano, Dec 11, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC nchini Marekani siku Bodi ya Utalii ilipotoa tuzo kwa mabalozi hao wanaotangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani. Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akiwashukuru mabalozi wa Utalii kabla ya kukabidhiwa tuzo zao kwa kazi nzuri wanaoifanya kwani sasa hizi Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka watalii wengi nchini Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi akiongea machache kuelezea vivutio vingine vyilivyopo hifadhi za Taifa za wanyama pori na kuwashukuru Mabalozi hao kwa kazi nzuri ya kutangaza Utalii wa Tanzania. Karen Hoffman mwakilishi wa bodi ya Utalii nchini Marekani kutoka kwenye kikundi cha Broadford kilichopo New York nchini Marekani pia akiongea machache na kuwashukur...