TANZANIA TOURIST BOARD 2013 AWARDS PRESENTATION

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba akiongea machache kuwashukuru Mbalozi wa wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumatano, Dec 11, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC nchini Marekani siku Bodi ya Utalii ilipotoa tuzo kwa mabalozi hao wanaotangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akiwashukuru mabalozi wa Utalii kabla ya kukabidhiwa tuzo zao kwa kazi nzuri wanaoifanya kwani sasa hizi Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka watalii wengi nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi akiongea machache kuelezea vivutio vingine vyilivyopo hifadhi za Taifa za wanyama pori na kuwashukuru Mabalozi hao kwa kazi nzuri ya kutangaza Utalii wa Tanzania.
 Karen Hoffman mwakilishi wa bodi ya Utalii nchini Marekani kutoka kwenye kikundi cha Broadford kilichopo New York nchini Marekani pia akiongea machache na kuwashukuru mabolozi hao kwa kazi yao ya kutangaza Utalii wa Tanzania hapa Marekani na juhudi zao kuzaa matunda na kuifanya Marekani kuongoza kwa kupeleka Watalii wengi nchini Tanzania.
 Mhe. January Makamba akimkabidhi tuzo mwakiishi wa Precision Air Bwn. Gregg Truman kama Balozi wa Utalii toka New York.
IMG_1709
 Mhe. January Makamba akimkabidhi tuzo Bi. Ally Miola kutoka Premier Traveler Magazine kama Balozi wa Utalii toka New York.
 Mhe. January Makamba akimkabidhi tuzo Bwn.Allan Feldstein kama Balozi wa Utalii toka California..
  Bwn.Allan Feldstein akitoa shukurani zake
Macon Dunnagan “Mr Kilimanjaro” akiongea machache nakuwashukuru Naibu Waziri, Mhe. January Makamba akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula, Bwn. Dunnagan ameisha panda Mlima Kilimanjaro mara 32.
Mhe. January Makamba, Mhe. Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Mabalozi wengine wanaotangaza utalii wa Tanzania nchini Marekani kwenye picha kutoka kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Tanzania National Park Bwn. Allan Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula, Bwn. Michael Boufield, Bwn. Roberto Parada, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba na Bwn Macon Dunnagan “Mr. Kilimanjaro”
Picha ya Pamoja Mhe. January Makamba na Balozi Liberata Mulamula wakiwemo Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania waliokuwepo kwenye Hafla hiyo. Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB