Posts

Showing posts from September 7, 2014

KESI YA TUNDU LISSU KUHUSU GHARAMA ZA UCHAGUZI HUKUMU SEPTEMBA 20

Image
Kesi ya madai ya gharama za uchaguzi anayodai Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu(chadema), inatarajiwa kutolewa hukumu Septemba 30 mwaka huu. Katika kesi hiyo namba 11 ya 2013, Lissu anadai gharama za uchaguzi za uendeshaji kesi katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambazo alishinda na kubaki na ubunge wake. Lissu anadai Sh. milioni 79 ikiwa ni  gharama za kesi ya uchaguzi aliyofunguliwa na Shaban Selema na Paschal Halu waliopinga ushindi wa ubunge wake. Baada ya kushinda kesi ya ubunge, Lissu aliiomba mahakama aweze kulipwa fedha hizo. Kesi hiyo ilisikilizwa Jana mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Dodoma, Rutatinisigwa, huku mdaiwa wa pili, Halu akiwakilishwa na wakili wa utetezi Geofrey Wasonga ambaye anapinga madai hayo na kusema njia iliyotumika si sahihi kulingana na viambatanisho vilivyowasilishwa mahakamani kughushiwa. Kwa hisani ya http://chademablog.blogspot.com/

EA Sports Release FIFA 15 Player Ratings: Messi Ahead of Ronaldo Again.. Here are The Top 10

Image
Cristiano Ronaldo might have beaten Lionel Messi to the Ballon d’Or earlier this year, but the Barcelona man has gained a measure of revenge on his great rival by winning another accolade. With a score of 93 out of a possible 100 Messi tops the player ratings in video game FIFA 15, which is due for release in the UK on September 26. To get debate among fans raging in advance, makers EA Sports released a countdown of the top 50 players on the newest instalment of the popular franchise.   Messi came out on top, beating Real Madrid star Ronaldo (92) by just a single mark on the scoring system. Bayern Munich and Holland winger Arjen Robben was third with a total of 90. The ratings, which are based on performances in league and cup games over the past 365 days, determine what each virtual player is capable of when used on the game. Paris Saint-Germain striker Zlatan Ibrahimovic and Bayern Munich goalkeeper Manuel Neuer are ranked fourth and fifth on the new game, de...

VIJANA WEKENI MSISITIZO MASOMO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILI MUWE WAJUZI NA KULETA MAENDELEO NCHINI

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mh Benjamin William Mkapa akizungumza na wanasayansi vijana katika mkutano wa wanasayasi vijana uliofanyika hiv i karibuni jijini Dar es salaam. Baadhi ya wanasayansi wakiwa katika mkutano wa wanasayasi vijana uliofanyika hiv i karibuni jijini Dar es salaam. ……………………………………………………………. Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM. Vijana nchini hawanabudi kupenda kujifunza masomo ya Sayansi na teknolojia ili waweze kupata ujuzi na mitazamo katika sekta ya gesi ambayo inakuwa kwa kasi kubwa hapa nchini na Duniani kwa ujumla. Kiukweli sayansi na teknolojia inasadikiwa kuwa mihimili mikubwa ya sasa katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali kwani mambo mengi yenye kuhitaji haraka hutegemea sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa. Licha ya kuwepo kwa changamoto zinazozikabili baadhi ya nchi nyingi za Afrika katika kupata maendeleo ikiwa ni pamoja na kutowekeza katika sayansi na teknolojia, hali inayopelekea baadhi ya nchi nyingi kukosa Wataalam wa ku...

RAIS KIKWETE AKAGUA VIFAA NA ENEO MAALUMU KWA WAGONJWA WA EBOLA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi vifaa maalumu vinavyofanya kazi ya kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.PICHA NA IKULU Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi madaktari na wauguzi walivyo jiandaa kufanya ukaguzi wa abiria na kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jueb4: lius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. : Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa  wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo S...

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI WA RWANDA, AMWAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Rwanda nchini Tanzania Balozi Eugene Segore Kayihura na kumwapisha balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda Balozi Ali Iddi Siwa katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete pia amepokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Norway nchini Tanzania Bibi Hanne Marie Kaarstad.Pichani Balozi mpya wa Rwanda nchini Tanzania 8647-Akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete.Na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Rwanda Ali Idd Siwa 8827 akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro)