KESI YA TUNDU LISSU KUHUSU GHARAMA ZA UCHAGUZI HUKUMU SEPTEMBA 20

Kesi ya madai ya gharama za uchaguzi anayodai Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu(chadema), inatarajiwa kutolewa hukumu Septemba 30 mwaka huu.
Katika kesi hiyo namba 11 ya 2013, Lissu anadai gharama za uchaguzi za uendeshaji kesi katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambazo alishinda na kubaki na ubunge wake.
Lissu anadai Sh. milioni 79 ikiwa ni  gharama za kesi ya uchaguzi aliyofunguliwa na Shaban Selema na Paschal Halu waliopinga ushindi wa ubunge wake.
Baada ya kushinda kesi ya ubunge, Lissu aliiomba mahakama aweze kulipwa fedha hizo.
Kesi hiyo ilisikilizwa Jana mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Dodoma, Rutatinisigwa, huku mdaiwa wa pili, Halu akiwakilishwa na wakili wa utetezi Geofrey Wasonga ambaye anapinga madai hayo na kusema njia iliyotumika si sahihi kulingana na viambatanisho vilivyowasilishwa mahakamani kughushiwa.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB