Posts
Showing posts from May 19, 2013
SHAMIM MOHAMED ALIVYOTWAA TAJI LA REDD'S MISS MZIZIMA 2013
- Get link
- X
- Other Apps
Redd's Miss Mzizima 2013,Shamim Mohamed (kati) akipunga mkono muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa taji hilo katika shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.Wengine pichani ni Mshindi wa Pili,Munira Mabrouk (kulia) pamoja na Mshindi wa Tatu,Rehema Mpanda. Warembo wa Redd's Miss Mzizima walioingia katika hatua ya tano bora,wakiwa wamejipanga kusubiri kupatikana kwa mshindi. Redd's Miss Mzizima 2013,Shamim Mohamed (kulia) akikabidhiwa hundi ya dola 450 kutoka kwa Mamaa wa Mitindo,Asia Idarous. Wacheza shoo wa Twanga Pepeta wakifanya mambo yao jukwaani.
RAIS KIKWETE KUZINDUA MRADI YA UJENZI WA BARABARA YA DODOMA-IRINGA
- Get link
- X
- Other Apps
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI YAH: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUZINDUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA YA DODOMA – IRINGA YENYE UREFU WA KM 260 (SEHEMU ZA DODOMA – FUFU ESCARPMENT, FUFU ESCARPMENT – MIGORI NA MIGORI – IRINGA) KWA KIWANGO CHA LAMI TAREHE 22 MEI, 2013 Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba, tarehe 22 Mei, 2013 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara kama ifuatavyo:- 1) Tarehe 22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu Escarpment (km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini. 2) Tarehe 22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu Escarpment – Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji cha Migori Wilayani Iringa Vijijini. ...
TASWIRA: UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA
- Get link
- X
- Other Apps
‘Chopa’ iliyotumiwa na Lema ikitua viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro muda mfupi kabla ya kuanza mkutano. Chopa hiyo ilizunguka anga la Jiji la Arusha kwa madoido ya aina yake, hususani katika Kata nne za Themi, Kimandolu, Elerai na Kaloleni, halikadhalika eneo la mkutano, huku ikimwaga vipeperushi vya kunadi kampeni za Chadema na wagombea wake. Blog hii ilishuhudia wananchi wakigombea vipeperushi hivyo vikitua chini. Sehemu ya umati wa wananchi wa Jijini Arusha waliojitokeza jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro kuhudhuria Mkutano Mkubwa wa Chadema wa Uzinduzi wa Kampeni za kuwania Udiwani kwa Kata nne zilizoachwa wazi na madiwani waliovuliwa uanchama na Chadema zaidi ya miaka miwili iliyopita. Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa kamati Kuu Chadema, Mh Godbless Lema akihutubia umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo. Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, ambae pia ni Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Arusha na Diwani wa Kata ya Levolosi, Mh Ephata Nanyaro...
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA ALLY SYKES JIJINI DAR
- Get link
- X
- Other Apps
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa marehemu Ally Sykes, Zainab Ally, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa marehemu Ally Sykes, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiaga na Mzee, Harith Mwapachu na kulia ni Balozi. Paul Rupia wakati wakati alipokuwa akiondoka baada ya kuhani msiba wa mwasisi wa TANU, Ally Sykes, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa kuzikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
PAMBANO LA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA LAINGIZA MIL 500/-
- Get link
- X
- Other Apps
Na Boniface Wambura, TFF Pambalo la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000. Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ...
VURUGU ZAIBUKA MJINI IRINGA KATI YA POLISI NA WAMACHINGA
- Get link
- X
- Other Apps
UVCCM Mbeya na Umoja wa Wanawake (UWT) Watoa matamko makali kupinga kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na Mkewe juu ya Raisi Jakaya Kikwete
- Get link
- X
- Other Apps
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya wametoa matamko makali kupinga kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na Mkewe juu ya Raisi Kikwete. Matamko hayo yalitolewa na Wenyeviti hao katika Mkutano na Vyombo vya habari uliofanyika katika Ofisi za UVCCM Mkoa wa Mbeya, ambapo walisema kamwe hawawezi kufumbia macho maneno ya uzushi na uchonganishi kati ya Serikali na wananchi. Akisoma tamko Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna alisema Umoja wa Vijana hauko tayari kufumbia macho matusi anayotukanwa Raisi Kikwete na Dk Slaa anapokuwa akihutubia wanachama wake jukwaani. Alisema katika Mkutano alioufanya Mei 12, Mwaka huu Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya Dk. Slaa akihutubia wananchi kuwa Raisi Kikwete ni Freemason, Mdini, Mawaziri hawamsaidii pia ni Mafisadi na kuongeza kuwa ana ushahidi wa Cd ambazo Raisi Kikwete akihamasisha udin...