MONGELLA ATUNUKIWA TUZO YA UMAHIRI AFRIKA
Mhe Balozi Getrude Mongella Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba amemkabidhi tuzo ya umahiri katika uongozi Mhe Balozi Getrude Mongella kutokana na juhudi zake katika kuwakomboa wanawake wa Bara la Afrika. Hafla ya kukabidhi Tuzo hiyo ya miaka 50 ya Pan African Women’s Organization (PAWO) ilimefanyika leo (23/12/2013) Courtyard Hotel jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi wa Wizara waliongozwa na Katibu Mkuu Bibi Anna T. Maembe na kushirikisha wajukuu wa Balozi Mongela. Mhe. Sophia Simba alifafanua kuwa lengo la hafla hiyo ni kutambua utumishi wake na kumkabidhi Mheshimiwa Mongella Tuzo ya heshima ya Wanawake Mashuhuri Barani Afrika ambao walionesha uongozi uliotukuka katika kutetea umoja, haki na usawa wa wanawake. Awali tuzo hiyo ilitolewa k...