RAIS DR. JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA SIKUKUU YA KRISMASI KWA YATIMA
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (katikati) akimkabidhi Mwakilishi wa Makao ya Watoto Kurasini wilayani Temeke Bibi Beatrice Mgumiro mbuzi watatu, kilo 150 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa ni zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu kwa furaha.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto Ramadhani Yahaya (kulia) mbuzi wawili (2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu kwa furaha.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Msimbazi Sister Maria Silvana (kulia) mbuzi watatu, kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi WA Kituo cha Vosa Mission Hochimin Mugarura (kulia) mbuzi wawili, kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu.
Picha na MAELEZO, Dar es salaam