Posts

Showing posts from September 16, 2012

WAKAZI WA MBEYA WALIPOKEA VYEMA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 VIWANJA VYA SOKOINE MKOANI HUMO.

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Linah akiimba kwa hisia jukwaani  ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya.   Wasanii wa Filamu hapa nchini Aunt Ezekiel,Wema pamoja na Shilole wakiwasikiliza mashabiki wao wanataka nini. Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Diamond akiwaimbisha mashabiki na wapenzi wa muziki huo waliojitokeza kwa wingi  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,kwenye uwanja wa Sokoine,mkoani Mbeya Msanii wa bongofleva kutoka THT,Barnaba akiwaimbisha mashabiki wake kwenye tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya. Msanii wa bongofleva Ben Paul akikamua vilivyo jukwaani. Recho kutoka THT akitumbuiza jukwaani  ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

JK azindua ujenzi wa daraja la Kigamboni

Image
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akiongea na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni uliofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik. Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli akimpa maelezo Rais Dtk.Jakaya Mrisho Kikwete juu ya Ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja hilo uliofanyika Kurasini jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete juzi, Alhamisi, Septemba 20, 2012, ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Dar es Salaam kwa kuwaonya watu ambao amewaeleza kuwa wanavyo viwanda vya kutunga uongo kuacha tabia hiyo na kuelekeza nguvu kwenye maendeleo. Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia wakazi wote wa Kigamboni ambao wanaondolewa katika maeneo yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa daraja hilo na ujenzi wa Mji Mpya wa Kigam...

Rufaa ya Lema yasogezwa mbele hadi Oktoba 2 mwaka huu

Image
   Picha juu na chini  ni Msafara wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema ukitokea mahakamani mkoani Arusha kuelekea ofisi za chama huku ukisindikizwa na umati wa wafuasi wa CHADEMA baada ya kuahirishwa kwa kesi inayomtuhumu. Gari ya Godbless Lema ikisukumwa na wafuasi wa CHADEMA kuelekea ofisi za Chama mkoani humo. (Picha na  http://woindeshizza.blogspot.com )

Mji wa Kismayo unakaribia kutekwa

Image
Wanajeshi wa Kenya wakipambana na Al-Shabaab Msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir anasema kuwa wanakaribia kuuteka mji wa bandarini wa Kismayo. Meja Chirchir amekariri kuwa wapiganaji wa Kenya wanaopigania kundi la Al Shabaab ikiwa wataweza kujisalimisha watasamehewa Kumekuwa na ripoti kuwa wapiganaji wa al-Shabaab wamenza kuutoroka mji huo katika siku chache zilizopita baada ya kuzingirwa na majeshi ya muungano wa Afrika kutoka pande zote Mji huo ndio ngome ya mwisho ya Al-Shabaab, ambayo huitumia kwa kuingza silaha na zana za kivita kutoka nchi za kigeni. Muungano wa Afrika unasema kuwa wanajeshi wa Somalia wameuteka mji wa Janaa Cabdlla ngome nyingine ya wapiganaji hao iliyo umbali wa kilomita hamsini Magharibi mwa Kismayo BBC SWAHILI

LEMA :SEREKALI ISITUGOMBANISHE CHADEMA NA WAMACHINGA ARUSHA

Image
  Aliyekuwa mmbunge wa jimbo la arusha mjini Godbless Lema kulia akiwa anaongea na waandishi wa habari kushoto kwake ni aliyekuwa mwanachama wa chama cha mapinduzi ambaye alijivua gamba nakuamia chadema James ole milya ,huku katika kati ni Katibu wa mkoa  chama cha demokrasia na maendeleo chadema  Gulkugwa Amani wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho uliohusiana na kuhairisha kwa mkutano uliokuwa ufanyike jana.   James ole milya akiongea katika mkutano huo ambapo alisisitiza na kuitaka serekali irejeshe viwanja vyote vya michezo vinavyomilikiwa na CCM kwani viwanja hivyo vimejengwa kwa kutumia fedha za wananchi na sio za chama hicho ,ambapo alitaja baadhi ni pamoja na kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid,Nyamagana kilichopo mwanza pamoja na kiwanja cha CCM kirumba Katibu wa mkoa wa chama cha demokrasia  Gulkugwa Amani na maendeleo chadema akiwa anasisitiza jambo wakati wa mkutnao wao na waandishi wa habari Ali...

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 NDANI YA JAMHURI MJI KASORO BAHARI MOROGORO

Image
Pichani kulia ni Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh Joel Bendera ambaye ni mgeni rasmi ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakati tamasha la Serengeti likiendelea kufanyika.  Pichani mbele ni msanii Rich Mavoko akiliongoza kundi lake jukwaani.  Ommy Dimpoz pichani kati sambamba na kundi lake wakitumbuiza kwenye jukwaa la Fiesta.  Mkali wa R&B Ben Paul akiwaimbisha wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Jamhuri. Msanii wa bongofleva Linah akitumbuiza jukwaani. Msanii mahiri katika mahadhi ya Mduara AT akiduarika na mmoja wa densa wake jukwaani. Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Recho akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro,ambapo wakazi kibao wa mji huo (hawapo pichani) wamejitokeza kwa wingi. Mmoja wa sanii chipukizi katika ...

Serengeti Fiesta 2012 Dodoma funika mbayaaaa!!!

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,mahiri katika miondoko ya miduara,AT akimrusha kimduara duara shabiki wake jukwaani huku shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala kutoka kwa watazamaji. Wasanii mahiri wa filamu hapa nchini nao walikuwepo kuliunga mkono tamasha la Fiesta ndani ya Dodoma,kutoka kulia ni Jacob Steven a.k.a JB,Wema Sepetu pamoja Aunt Ezekiel. Ray Kigosi akilicheza sebene jukwaani. Ray akimtambulisha Wema Sepetu kwa mashabiki. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Dr Rehema Nchimbi akisoma jina la mshindi wa gari aina ya Vitz inayotolewa na kampuni ya Push Mobile,ikiwa ni sehemu ya mchakato wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani kati ni Meneja masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rodney Lugambo,Muwakili shi wa michezo ya bahati nasibu ya Taifa,Bwa.Humudi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Mh Lephy Gembe.   Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Mh Lephy Gembe akiwasalimia wakazi wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi  kwenye tamasha la Serengeti Fies...

Brigit Alfred aibuka kidedea Redds Miss Kinondoni 2012

Image
Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana George Hussein na mshindi watatu Irene David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza 2012 huku Irine akishikilia taji la Miss Ubungo 2012.  Warembo hao wakiwa kwenye vazi la ufukweni wakipita mbele ya majaji na watazamaji walioshuhudia shindano hilo.  Mshindi aliyenyakua taji hilo Brigit Alfred akicheza midundo ya kihindi kwenye kinyang'anyiro cha vipaji na kuibuka kidedea. Hawa ndio waliofika tano bora kutoka kushoto ni, Judith Sangu, Brigit Alfred, Diana George Hussein, Irene David na Kudra Lupatu. Judith Sangu akionyesha uwezo wake wa kucheza muziki kwenye Miss Tallent.