Brigit Alfred aibuka kidedea Redds Miss Kinondoni 2012


Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana George Hussein na mshindi watatu Irene David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza 2012 huku Irine akishikilia taji la Miss Ubungo 2012.


 Warembo hao wakiwa kwenye vazi la ufukweni wakipita mbele ya majaji na watazamaji walioshuhudia shindano hilo.





 Mshindi aliyenyakua taji hilo Brigit Alfred akicheza midundo ya kihindi kwenye kinyang'anyiro cha vipaji na kuibuka kidedea.





Hawa ndio waliofika tano bora kutoka kushoto ni, Judith Sangu, Brigit Alfred, Diana George Hussein, Irene David na Kudra Lupatu.

Judith Sangu akionyesha uwezo wake wa kucheza muziki kwenye Miss Tallent.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB