Posts

Showing posts from October 14, 2012

VURUGU ZILITOKEA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
         Maeneo ya Kariakoo njia na barabara zote zilikuwa nyeupeeee kama hivi...  Njia zote za kwenda na kurudi yalikuwa yakitamba magari ya polisi tu.  Askari wakikagua paspoti ya Raia wa kigeni, ili kumruhusu kupita maeneo hayo....Posta mpya.  Daladala ziliamuliwa kubadili na kupita njia nyingine.....  Askari wa doria ya pikipiki wakikatiza katika mitaa ya Posta Mpya.... Askari wa Mbwa wakiimarisha ulinzi.  

Waziri Mkuu akutana na Watanzania nchini Uingereza

Image
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mh. Peter Kallaghe wakati akiwasili kwenye ofisi za Ubalozi nchini Uingereza alipofika kukutana na kuzungumza na Watanzania waishio nchini humo.Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda. Siku ya jumanne tarehe 16.10.12 Mh Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mizengo Kayanza Peter Pinda alipata fursa ya pekee ya kukutana na baadhi ya watanzania waishio nchini Uingereza katika ofisi za Ubalozi wetu zilizopo hapa jijini London ili kuongea, kufahamiana nao na kuwapa taarifa kamili kuhusu hali ya nchi Kiuchumi, Kisiasa, Kiusalama, Kimaendeleo na changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa letu. Mh Waziri Mkuu alieambatana na mkewe mama Tunu Pinda walipokelewa rasmi na Mh Balozi wetu Peter Kallaghe, wafanyakazi pamoja na maofisa kutoka ngazi mbalimbali katika Ubalozi wetu. Kabla ya kuanza hotuba yake Mh Balozi alichukua fursa hii kuwakaribisha na kuwashukuru watanzania wote ambao wal

MASWALI MENGI YAIBUKA KIFO CHA KAMANDA WA POLISI MWANZA

1.  Endelea kufananisha picha. Lakini endelea pia kujenga mashaka kama nilivyoandika siku mbili zilizopita. 2.  Kamanda alikuwa anatoka wapi - sherehe? 3.  Alimbeba nani - mwalimu? Lifti? Kutoka wapi kwenda wapi? Mwalimu alikuwa anatoka wapi usiku huo? Hajaolewa? Mume wake yuko safari au alighairi sherehe? Mume wa mwalimu ni nani? Wanaishi wapi? Alimwacha wapi mume wake na kubebwa na polisi mkuu wa mkoa? Aliwaacha wapi aliokuwa nao na yeye kupata lifti? Kwanza kabisa, alikuwa na nani kabla hajapewa lifti. Mtu wa mwisho kumwona mwalimu na polisi wakiondoka ni nani? Kama polisi alipakia abiria wengine walishuka wapi? 4.  Mkuu wa polisi na mwalimu walikuwa pamoja kwa muda gani wakiwa peke yao na wapi? A La Kairo au wapi? Hapo Kairo walikuwa wakifanya nini - tangu lini hadi lini? Mwalimu wa shule ya msingi ya Nyamagana, eti? Alikuwa anatoka wapi - naye kwenye sherehe hiyohiyo na Burlow? 5.  Mwalimu mkuu anasema nini? Dada yake? Ndugu zake wengine? Hivi polisi mkuu wa mkoa na mwalimu waliku

TANZANIA AND THE SULTANATE OF OMAN SIGNED VARIOUS AGREEMENTS AIMED AT ENHANCING POLITICAL AND ECONOMIC

Image
Tanzania and  The Sultanate of Oman yesterday signed various agreements aimed at enhancing political and economic ties between the two countries. The Agreements were signed during the second day of President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete’s State Visit to the Sultanate following the invitation of His Majesty Sultan Qaboos  bin Said Al Said. The agreements  were signed yesterday during the joint Tanzania- Oman business forum held at AL Bustan Hotel in Muscat Oman including, The Agreement on Promotion and Protection of Investment, Memorandum of Understanding on Cooperation in higher Education between Oman and Zanzibar, Agreement on Cooperation in Records and Archives and the Agreement on Forming joint Business Council between Oman and Tanzania. In the Pictures below. The Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Bernard Membe and Oman Ministry of Financial Affairs Secretary General, Sultan bin Salim Al Habsi signing legal instruments on the Agreement on Promotion and  P

UMOJA WA ULAYA WAWEKA WAZI NIA THABITI YA KUKUZA SEKTA YA NISHATI NCHINI TANZANIA

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa unaoshughulikia Matumizi endelevu ya Nishati kwa wote, wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa rais, Ikulu jijini Dar es   Salaam, leo Oktoba 17, 2012 kwa mazungumzo. (Picha na OMR). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa kutoka Umoja wa Mataifa unaoshughulikia Matumizi endelevu ya Nishati kwa wote, wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa rais, Ikulu jijini Dar es   Salaam, leo Oktoba 17, 2012 kwa mazungumzo .  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na (Mshauri wa Nishati Umoja wa Ulaya), Bw. Luis Gomez Echeverri, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 17, 2012. Kushoto ni Faouzi Bensarsa (Mshauri wa Nishati Umoja wa Ulaya) . (Picha na OMR) . Mheshimiwa Makamu w

MH. PINDA AKIWA JIJINI LONDON

Image
    Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza kabla ya kuzungumza na watanzania waishio nchini Uingereza jijini London . Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe.  Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akitazama kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza uliopo London kuzungumza na Watanzania waishio Uingereza. Kushoto ni mkewe Tunu na kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe.     Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa na Mtangazaji wa Shirika la Habari la Uingereza BBC Zawadi Machibya (kulia) wakati alipozungumza na Watanzania waishio Uingereza kwenye Ubalozi wa Tanzania uliopo London. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

VURUGU ZANZIBAR ZA CHUKUA SURA NYINGINE, ASKARI AUAWA KINYAMA KUFUATIA VURUGU ZA WAFUASI WA UAMSHO

Image
  Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi wa Habari akielezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.   Mwandishi wa Habari wa Hits FM Mustafa akiuliza maswali katika Mkutano wa Jeshi la Polisi juu ya fujo na ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi,hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar. Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano wa Jeshi la Polisi kuelezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar. Na Ramadhan Ali na Mwanaisha Mohammed -Maelezo Zanzibar .  Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati ak

SULTANI QABOOS WA OMAN AMTUNUKU NISHANI YA HESHIMA RAIS DKT.JAKAYA KIKWETE

Image
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman jana jioni muda mfupi kabla ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake.  Sultani wa Oman,Qaboos bin Said Al Said akimtunuku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nishani ya juu ya heshima, Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya  AL Alam jijini Muscat Oman. Sultan Qaboos bin Said Al Said akimpongeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman juzi jioni katika kasri ya AL Alam. Jijini Muscat Oman jana jioni .Rais Kikwete aliwasili nchini Oman jana jioni kwa ziara rasmi ya siku nne. (Picha na Freddy Maro)

WASHIRIKI REDDS MISS TANZANIA 2012 WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL ARUSHA

Image