Posts

Showing posts from February 10, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASIMAMIA ZOEZI LA UTEKETEZAJI SILAHA HARAMU JIJINI DAR LEO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivuta waya kuashiria kufyatua mtego wa kuwasha moto wa kuteketeza Silaha haramu, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo la uteketezaji wa silaha haramu, Lililofanyika katika Kambi ya Magereza jijini Dar es Salaam, Jumamosi Feb 16, 2013. Kushoto kwake ni Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Siro na wa pili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Perera Ame Silima na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kmataifa, Benard Membe. Sehemu ya Silaha hizo zikianza kuteketea kwa moto baada ya Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufyatua waya maalumu wa kuwasha moto huo. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, baada ya kusimamia zaoezi la uteketezaji wa Silaha haramu, lililofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moh

JK AONGOZA MAELFU KUMZIKA ASKOFU LAIZER

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Mstaafu awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa wakishiriki ibada ya Mazishi ya Askofu Dkt.Thomas Laizer iliyofanyika katika kanisa na Usharika wa mjini Kati.mjini Arusha jana. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Maua katika kaburi la Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer wakati wa mazishi yaliyofanyika katika Kanisa KKKT Usharika wa mjini Kati,Arusha mjini jana. Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA  na Freeman Mbowe  Mbunge wa Jimbo la Hai Mh.  kwenye mazishi ya ya Askofu Thomas Laizer jana katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati. Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Askofu Dk. Alex Malasusa akiongoza ibada ya Mazishi ya Askofu Thomas Laizer jana katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati,jijini Arusha. Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya

MJUMBE WA NEC YA CCM, MAMA SALMA KIKWETE ZIARANI LINDI MJINI

Image
     

RAIS KIKWETE ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU ASKOFU THOMAS LAIZER WA KKKT

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo, Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na waumini wa Dayosisi ya Kaskazini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuuaga mwili wa askofu wa jimbo hilo, Askofu Dkt. Thomas Laizer. Rais Kikwete na uju mbe wake amewasili kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kiasi cha saa 10:50 akaenda moja kwa moja kuaga mwili wa Marehemu Laizer na baadaye akakuta na kuwafariji wafiwa akiwamo Mke wa Askofu Laizer, Mama Maria Laizer. Rais pia atashiriki mazishi yake yaliyopangwa kufanyika kesho, Ijumaa, Februari 15, 2013 katika Kanisa Kuu hilo la KKKT la mjini Arusha. Askofu Dkt. Thomas Olmorijoi Laizer ambaye alizaliwa Machi 10, mwaka 1945 katika Kijiji cha Engarenaibor, Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha alifariki dunia Alhamisi iliyopita, Februari 7, majita ya saa 12 jioni kwa magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la Damu.

RAIS KIKWETE ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU ASKOFU MSTAAFU JIMBO KATOLIKI MOSHI MHASHAMU AMEDEUS MSARIKIE

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la Askofu Mtsaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu Mfalme, mjini Moshi leo. ( PICHA NA FREDDY MARO WA IKULU) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Moshi na kutoka sehemu nyingine nchini, kumzika Askofu Mstahivu (Bishop Emeritus) Amedeus

PINDA AKUTANA NA MKURUGENZI WA WFP NA UJUMBE WABUNGE WA UJERUANI

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi  Mtendaji  wa Mpango wa Chakula  Duniani (WFP), Bibi Ertharin Cousin Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 13, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya bunge la Ujerumani walipomtembelea, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 13, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya bunge la Ujerumani baada ya kuzungumza nao, Ofisini kwake Februari 13, 2012.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi. (PIcha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

RAIS KIKWETE KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA POLISI

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt.Emmanuel Nchimbi pamoja na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Saidi Mwema muda mfupi baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma juzi jioni. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dr Jakaya Mrisho Kikwete, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka kwa maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi juzi jioni katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni, mjini Dodoma. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.    Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dr Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IJP Saidi Mwema alipokua anawasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma alipokwenda kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi juzi jioni.Kauli mbiu ni “Tujenge Uwezo wa Jamii na Polisi Kukabiliana na Vurugu kwa Kuimarisha Utii wa Sheria Bila Shuruti”. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi

JULIANA SHONZA NA MTELA MWAMPAMBA WAJIUNGA NA CCM

Image
Juliana Shonza akijitambulisha kwa wana CCM jana tarehe 12/2/2013, katika Makao Makuu ya CCM,mjini Dodoma Mtela Mwampamba akijitambulisha kwa wana CCM,wakati wa sherehe za utambulisho wa  wajumbe wa kamati kuu ya CCM. Mwenyekiti wa CCM-Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wapya  wa CCM,Juliana Shonza na Mtela Mwampamba,kushoto kwenye picha ni Makamu Mwenyekiti CCM-Bara ,Ndugu Philip Mangula na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahaman Kinana. Mwenyekiti wa CCM-Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa Dodoma wakati wa sherehe za kuipongeza Kamati Kuu iliyochaguliwa jana mjini Dodoma.

LOWASA, SUMAYE WAMFARIJI MKURUGENZI CRDB DK KIMEI KUFUATIA KIFO CHA MAMA YAKE MZAZI

Image
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akiwapa pole Dr Kimei(katikati) na dada yake. Pichani ni Mawaziri wakuu wastaafu Mh Edward Lowassa na Mh Fredrick Sumaye wakijumuika na viongozi wengine katika msiba wa mama yake mkurugenzi mtendaji mkuu wa CRDB, Dr.Charles Kimei mwishoni mwa wiki huko Komakundi Marangu Mkoani Kilimanjaro.

ASKOFU THOMAS LAIZER KUZIKWA IJUMAA HII ARUSHA

Image
ALIYEKUWA Askofu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer anatarajiwa kuzikwa Ijumaa ya keshokutwa  Februari 15, 2013. Kwa Mujibu wa Taarifa maalum iliyotolewa na Kamati ya Mazishi ya KKKT na Familia ya Marehemu, inasema kuwa Marehemu atazikwa katika eneo la Kanisa Kuu mjini Kati Arusha. Aidha taarifa hiyo ambayo Father Kidevu Blog imeipata inasema kuwa waumini na Washirika wa Kanisa Kuu na makanisa yote ya KKKT nchini, Wananchi, ndugu jamaa na marafiki watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa marehemu kuanzia Alhamisi Alasiri ya Februari 14, 2013. Taarifa hiyo iliongeza kuwa Mwili wa Askofu Laizer utalala Kanisani hapo hadi Ijumaa ya Mazishi. Marehemu Askofu Thomas Laizer aliyezaliwa Machi 10, 1945 katika Kijiji cha Kitumbeni Arusha na baade kupata elimu yake ya msingi hadi darasa la nane Longido na kumaliza mwaka 1965. Askofu Laizer, aliendelea na masomo yake ya juu ndani na baade

MHESHIMIWA RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA NEC DODOMA LEO

Image
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, kabla ya kuanza kikao hicho leo.  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisahuriana jambo ukumbini na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo  Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akimsalimia Katibu wa NEC Siasa ana Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya kikao kuanza ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  Hali ndani ya ukumbi ilikuwa kama hivi kabla ya kikao kuanza. Kushoto Kabisa ni Nape na Zakia Meghji na juu-kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wajumbe. Na Kulia chini ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhamed Seif Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakiteta jambo