RAIS KIKWETE ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU ASKOFU MSTAAFU JIMBO KATOLIKI MOSHI MHASHAMU AMEDEUS MSARIKIE


8E9U0007Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo.
8E9U0062Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo.
8E9U9885Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la Askofu Mtsaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu Mfalme, mjini Moshi leo. (PICHA NA FREDDY MARO WA IKULU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Moshi na kutoka sehemu nyingine nchini, kumzika Askofu Mstahivu (Bishop Emeritus) Amedeus Peter Msarikie.
Rais Kikwete amewasili  kwenye Kanisa Kuu la Kristo Mfalme mjini Moshi kiasi cha saa sita na dakika tano mchana kuungana na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na mamia kwa mamia wananchi kwa ajili ya mazishi ya Askofu Msarikie ambaye alifariki dunia Alhamisi iliyopita, Februari 7, 2013 kwa ugonjwa wa saratani katika hospitali moja mjini Nairobi, Kenya.
Mara baada ya kuwasili, Rais Kikwete ametia saini kwenye kitabu cha maombolezo na ikaanza ibada ya mazishi ilivyohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi wakiwamo maaskofu zaidi ya 20 kutoka majimbo mbali mbali ya Kanisa Katoliki nchini.
Mwili wa Marehemu Msarikie uliteremshwa kaburini kiasi cha saa saba na dakika 35 ndani ya Kanisa hilo na Rais Kikwete akaweka udogo kwenye kaburi na baadaye shada la maua.
Akizungumza kwenye mazishi hayo, Rais Kikwete amemwelezea Askofu Msarikie ambaye alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi kwa miaka 26 kama “kiongozi shupavu wa kiroho ambaye aliwalea vyema kondoo wa bwana. Lakini pia alikuwa kiongozi hodari  kwa maendeleo ya jamii yaliyowanufaisha waumini wake na hata wale wa madhehebu na dini nyingine.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Kwa kweli sote tumepoteza mtu muhimu. Tunamfahamu marehemu Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowatendea watu wa jimbo lake, ya kiroho na ya maendeleo. Mimi binafsi, wana-moshi na Watanzania kwa ujumla tutamkumbuka na kumuenzi Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowafanya wanadamu wenzake na nchi yetu.”

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB