Posts

Showing posts from October 7, 2012

WEALTHY CEO THREATENS TO FIRE EMPLOYEES IF PRESIDENT OBAMA IS RE-ELECTED

Image
  Heard about the multi-millionaire CEO who is building the largest house in America, and told his employees in a lengthy e-mail that he was going to fire them if President Barack Obama gets re-elected? That guy’s a real jerk, right? According to  Gawker , David Siegel — founder and CEO of Westgate Resorts, a huge national timeshare and one of the largest resort developers in the world — used to be a billionaire, but after the economic recession, he got downgraded to a hundred-millionaire. (Poor him, right?) He and his wife Jackie recently appeared on the documentary “ Queen of Versailles ,” which covered the couple’s rags-to-riches story and their ongoing quest to construct the largest house in America — a 90,000 square foot reminder of their massive fortune. And now, after losing so much money — because of, you know, the recession, and NOT his extravagant, over-the-top lifestyle — Siegel, a staunch Republican, has politely...

MAKAMU WA RAIS BENKI YA DUNIA AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA

Image
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar Diop kulia ,akiwa ameambatana na  Maafisa  Waandamizi kutoka Benki ya Dunia wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe. William  Mgimwa hayupo kwenye picha. Balozi wa Tanzania nchini Japan  Bi. Salome Sijaona kushoto akifuatiwa na Dk. Servacius B. Likwilile Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akifuatiwa na  ni Mhe. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa na  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa Omari walioko nyuma ni maafisa waandamizi  wa Tanzania Jijini Tokyo – Japan wakimsikiliza kwa makini Bw. Makhtar Diop, ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika. Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa pamoja na maafisa kutoka Benki ya Dunia wakiendelea na majadiliano juu ya kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania ili iweze kendelea kiuchumi hapa Jijini Tokyo- Japan. Kushoto kwa Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu...

Rais Kikwete aifariji familia ya Marehemu Walid Juma

Image
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji  na kuomba dua pamoja na familia ya  aliyekuwa kamishna wa Ushuru wa Foradha TRA Marehemu Walid Juma nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Walid  amezikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini dare s Salaam.  Picha na Freddy Maro

JUST IN: KUUWAWA KWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ,IGP MWEMA ATUMA KIKOSI MWANZA

Image
                            RPC Mwanza aliyeuwawa Liberatus Barlow   Mkuu  wa  jeshi la  polisi (IGP) Said Mwema amethibitisha  kuuwawa kwa kakamnda  wa  Mwanza Liberatus Barlow . Amesema  kuwa  kamanda  huyo wa polisi ameuwawa na  watu  wanaosadikika kuwa ni majambazi majira ya saa 7.30  na saa 8 usiku   katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza. Mwema amesema  kuwa kamanda  Barlow alikuwa akitokea katika  kikao cha harusi akiwa njiani kumrudisha dadake nyumbani kwake ghafla  alikutwa na tukio  hilo la  kupigwa  risasi. Hata  hivyo alisema  kuwa  kutokana na tukio  hilo jeshi la  polisi  linataraji kuanza uchunguzi  wake kuanzia leo na timu ya askari  kutoka  makao makuu ya polisi  wataondoka mapema leo kwenda  jijini Mwanza...

MWANADADA JOKATE MWEGELO JOKATE AZINDUA RASIMI KAMPUNI YAKE YA "KIDOTI LOVING"

Image
Mrembo, mtangazaji na mjasiriamali wa nchi Tanzania Jokate Mwegelo leo ameizundua rasmi kampuni yake ya Kidoti Loving katika hafla iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Bidhaa za kwanza za Kidoti zilizoingia sokoni ni Nywele (weaving) ambazo amesema tayari zinapatikana katika soko la Kariakoo na maeneo mengine jijini Dar es Salaam ambapo baada ya muda mfupi zitaanza kupatikana mikoani.

WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO

Image
Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakiwa nje ya jengo la Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro walikofika kujionea vivutio mbalimbali katika bonde la hifadhi hiyo ambalo lina mambo mengi ya ajabu miongoni mwa hifadhi. Mbali na kujionea wanyama wa aina mbalimbali na ndege pia warembo hao walipata fursa ya kujifunza juu ya Bonde hilo ambalo lipo katika mchakato wa kuingia katika Maajabu ya dunia. Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja na Watalii waliofika katika Bonde la Ngorongoro kujionea vivutio mbali mbali. Baadhi ya warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakipewa maelezo juu ya picha mbalimbali za Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro, wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo kwa kujifunza na kujionea mambo mbalimbali. Warembo hao wa Redd's Miss Tanzania 2012 wapo Kanda ya Kaskazini kwa ziara ya kuhamasisha Utalii wa Ndani. Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzan...

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MFANYAKAZI WA OFISI YAKE

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, Jenkins Chochole Matulile, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani  kwao Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam, Oktoba 11, 2012. (Picha na OMR). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu,  Jenkins Chochole Matulile, aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani  kwao Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam, Oktoba 11, 2012. (Picha na OMR).  Makamu wa...

CHADEMA WAANZA MASHAMBULIZI SUMBAWANGA

Image

FREEMAN MBOWE AUNGURUMA JIJINI ARUSHA

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha. Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha katika muendelezo wa kampeni za chama chake kuwania nafasi ya uwakilishi katika Halmashauri ya Jiji kupitia Kata hiyo.  Mkutano huo nusura usifanyike hiyo jana baada ya kilichoelezwa kuwa chama hicho kilikosa eneo la kufanyia mkutano na hivyo kulazimiaka kufanyia nje ya ofisi za chama hicho Kata ya Daraja Mbili, ofisi ambazo ziko jirani na za mahasimu wao kisiasa, CCM.Aidha, ujio wa Mbowe haukujulikana mapema kiasi cha wananchi kushangaa kumuona jukwaani ghafla tu. Pia, Mh Mbowe hakuweza kumnadi mgombea wa chama hicho kwa kuelezwa kwamba alikuwa anashikiliwa na Polisi alikolazwa hospitali ya Mt Meru na hivyo kushindwa kuhudhuria mkutano huo. Godbless Lema nae akizungumza mkutanoni hapo. Juu na chin...

Chatanda amtunishia misuli Lowassa

Image
Edward Lowassa   SIASA za makundi ndani ya CCM, zimeendelea kujidhihirisha wazi baada ya katibu wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kukwepa kumtambulisha Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) kupitia Wilaya ya Monduli, Edward Lowassa aliyekuwa meza kuu.Tukio hilo la aina yake lilitokea jana wakati Chatanda akitambulisha wageni waalikwa na viongozi wa chama  na Serikali waliokuwa meza kuu katika mkutano wa uchaguzi wa nafasi ya  mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha. Mara baada ya Msema Chochote (MC) kumpa kipaza sauti Chatanda, alianza kwa kuwatambulisha viongozi hao na kuwapa nafasi ya kusalimia, lakini ilipofika kwa Lowassa alimruka na kumkaribisha Mwenyekiti wa Mkoa aliyemaliza muda wake, Onesmo Nangole ili kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano huo. Kutokana na hali hiyo, wajumbe wa mkutano huo, walianza kupaza sauti  huku wakisisitiza ‘bado mjumbe mmoja, bado mjumbe mmoja’  ndipo Chatanda alipomtambulisha Lowassa na kum...

Vurugu Mbagala

Image
Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia wakiwadhibiti vijana waliokuwa wakileta vurugu eneo la mbagala kufuatia kijana mmoja anaesemekana anasoma kidato cha kwanza kukojolea mkojo Quraan na kusababisha hasira kwa waisilamu hassa vijana ambao walitapakaa mitaani na kuanza kuleta vuru. Vijana waliosambaa mitaani na kuamsha vurugu kubwa kwenye eneo hilo la Mbagala Kizuiani. Hapa baadhi ya waisilamu walioamua liwalo naliwe nakuamua kuwatunishia msuli polisi nakusema pigeni mpendavyo hatoki mtu. Barabara zilikua zikiharibiwa kwa moto ulikuwa ukiwashwa na waisilamu hao wenye hasira. Maji ya kuwasha yalikuwepo ingawa hayakuweza kuzuia vurugu hizo. Askari na watuhumiwa wakivuka pamoja kwenye mtaro wa maji taka. Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi.  Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)