WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO


Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakiwa nje ya jengo la Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro walikofika kujionea vivutio mbalimbali katika bonde la hifadhi hiyo ambalo lina mambo mengi ya ajabu miongoni mwa hifadhi. Mbali na kujionea wanyama wa aina mbalimbali na ndege pia warembo hao walipata fursa ya kujifunza juu ya Bonde hilo ambalo lipo katika mchakato wa kuingia katika Maajabu ya dunia.
Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja na Watalii waliofika katika Bonde la Ngorongoro kujionea vivutio mbali mbali.
Baadhi ya warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakipewa maelezo juu ya picha mbalimbali za Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro, wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo kwa kujifunza na kujionea mambo mbalimbali. Warembo hao wa Redd's Miss Tanzania 2012 wapo Kanda ya Kaskazini kwa ziara ya kuhamasisha Utalii wa Ndani.
Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa pamoja na Watalii wengine wakioangalia maajabu ya Bonde la Ngorongoro ambalo ni moja ya vivutio vinavyotarajiwa kuingia kwenye maajabu ya Dunia.
Warembo wa Redd's Miss Tanzania Wakiwa kwenye Magari Maalum wakati wakiizungukia maeneo ya Bonde la Ngorongoro kujionea wanyama na ndege aina mbali mbali.
Warembo wakifurahia kutembelea hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB