Posts

Showing posts from September 8, 2013

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAONESHO YA NYARAKA ZA KITAIFA NA KUMBUKUMBU ZA OMAN

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka  kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Hifadhi ya kumbukumbu za Kitaifa za Oman Dk.t Hemed Mohammed Al-Dhawyani  kwenye ufunguzi wa maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia nyaraka za aina kumbukumbu mbalimbali kwenye maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman mara baada ya kufungua maonesho hayo leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Posted in  General  on  September 10, 2013 ...

RAIS DKT. KIKWETE AZURU WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA

Image
Mkuu wa Chuo cha Michezo cha Malya Ndugu Allen Alex akimwelezea rais Jakaya Kikwete ramani ya eneo lote la chuo mara tu baada ya uzinduzi wa uwanja wa ndani wa michezo. Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akiangalia  ngoma za utamaduni wa Kisukuma zilizokuwa zikicheza wakati Rais Jakaya Kikwete alipofika tu uwanjani hapo kwa ajili ya mkutano wa hadhara huko Ngudu tarehe 9.9.2013. Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa Ngudu muda mfupi kabla ya kuwahutubia. Rais Jakaya Kikwete akitawazwa na kusimikwa rasmi kuwa Kamanda  Mkuu wa sungusungu nchini  na Chifu Shimbi Martin Morgan wa wilaya ya Kwimba.Katika sherehe hiyo Rais Kikwete alikabidhiwa kofia nyekundu, mgolole, upinde na mshale pamoja na silaha nyingine za kijadi. Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Kwimba huko mjini Ngudu ili kuhitimisha ziara ya ya siku moja wilayani humo tarehe 9.9.2013.   PICHA NA JOHN LUKUWI 

PICHA ZA SERENGETI FIESTA 2013 IRINGA

Image
  Anaitwa Shilole na Skwadi lake wakilishambulia jukwaa vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake kwenye uwanja wa Samora,ambapo tamasha la Serengeti fiesta. Moja ya kikundi mahiri kutoka jijini Dar,chenye maskani yake Kinondoni,KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza moja ya wimbo wa Michael Jackson,mbele ya wakazi wa Iringa wakati tamasha la Serengeti fiesta  ndani ya uwanja wa Samora. Walter Chilambo akiimba jukwaani wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Samora.  Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani .   Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani  mbele ya maelfu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013. Linah,moja ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa Bongoflev...

Nguvu yako ni Mtaji.

Image
Jamaa mmoja ambaye jina lake halikufahamika mapema, akiwa amebeba gunia la vitungu lenye uzito zaidi ya 100Kg za vitunguu linalouzwa kwa Sh. 90,000/ = akitoka nje ya lango kuu la kutokea sokoni maarufa kama "Shimoni". ndani ya soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam.