PICHA ZA SERENGETI FIESTA 2013 IRINGA

 Anaitwa Shilole na Skwadi lake wakilishambulia jukwaa vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013

Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake kwenye uwanja wa Samora,ambapo tamasha la Serengeti fiesta.
Moja ya kikundi mahiri kutoka jijini Dar,chenye maskani yake Kinondoni,KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza moja ya wimbo wa Michael Jackson,mbele ya wakazi wa Iringa wakati tamasha la Serengeti fiesta  ndani ya uwanja wa Samora.
Walter Chilambo akiimba jukwaani wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Samora. 
Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani .

  Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani  mbele ya maelfu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

Linah,moja ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva akiimba kwa hisia jukwaani,huku shangwe za mashabiki zikivuma kila kona ya uwanja.
Rais wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,Madee akiwaimbisha mashabiki wake kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,linalofanyika ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Mmoja wa madansa machachari sana kutoka THT,aitwaye Msami akiwa amebebwa juu na mashabiki baada ya kuonesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma jukwaani.
Wasanii wanaokuja juu katika anga ya muziki wa kizazi kipya-hip hop.Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa kwa pamoja huku mayowe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB