FLAVIANA MATATA FOUNDATION YAZINDUA “FMF STATIONARIES PROJECT”
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Flaviana Matata Foundation (FMF) inafanya kazi ya kuhamasisha, kuwezesha na kusaidia wasichana nchini kwa kuwaelimisha na kuwapa misingi ya kuwajenga kuwa kati ya watendaji wazuri wanaochangia katika shughuli za maendeleo ya jamii. Ili kufanikisha hayo, FMF inawadhamini wanafunzi wasichana kwa kuwalipia ada za shule, kuwanunulia sare za shule pamoja na misaada mingine mbali mbali yenye kumwezesha mwanafunzi kusoma vizuri kuanzia elimu ya msingi, upili na hatimaye kufikia kwenye taasisi mbali mbali za elimu ya juu. Malengo makuu ya Flaviana Matata Foundation ni pamoja na: Kusaidia kuongeza idadi ya watoto wa kike wanaojiunga katika ngazi mbali mbali za elimu. Kuhamasisha harakati za kutokomeza umasikini Tanzania kupitia miradi mbali mbali ya elimu. Kuhamasisha wasichana kujiendeleza kufikia elimu ya juu pamoja na elimu ya ufundi. Kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za kijasiriamali. Katika kufikia malengo hayo, Flaviana ...