POLISI WAREJESHA VITITA VYA FEDHA ZA WACHINA VILIZOIBWA KATIKA TUKIO LA UTEKAJI


kamanda_4f88e.jpg
"Jamani pesa yenu iliyoibiwa hii hapa," Ni kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Athmani Mungi akiwaonyesha raia wa China maburungutu ya fedha zilizonusurika kutoka kwa majambazi waliowateka na kuwapora raia wa China.
fedha_9623f.jpg
Fedha shilingi Milioni 80 ambazo zimerejeshwa na jeshi la polisi kutoka mikononi wa majambazi wa tukio la utekaji wa raia wa Kichina, waliovamiwa katika mlima wa Nyang'olo mkoani Iringa.
silaha_e88e3.jpg
Kamanda Mungi akiwa ameshika Silaha aina ya ShortgunGreener ambayo imekatwa Mtutu (kitako) silaha iliyotupwa na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi baada ya kuzidiwa nguvu na askari polisi katika mapambano ya kuokoa fedha za raia wa China.
mamilioni_f716e.jpg
Mamilioni ya fedha yakiwa yameshikwa na kamanda wa jeshi la Polisi mkoni Iringa, mara baada ya kusalimika kutoka mikononi mwa majambazi, ambao walipora vitita vya fedha hizo kutoka kwa raia wa China.
raia_65da1.jpg
Raia wa China wakiwa na askari polisi katika ukumbi wa ofisi ya kamanda wa jeshi la polisi wakipewa taarifa za kupatikana kwa baadhi ya fedha zao na vifaa walivyoporwa na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi.
raiaaa_21526.jpg
Raia wa China wakiwa katika ofisi ya kamanda wa jeshi la Polisi mko wa Iringa, wakifurahia kuziona fedha zao ambazo zilikuwa zimepolwa na majambazi katika mlima wa Nyang'olo Wilaya ya Iringa, wengine ni askari wa jeshi la Polisi.

Popular posts from this blog

MH. AMANI ABEID KARUME AFUNGUA SKULI YA DONGE ZANZIBAR