Posts

Showing posts from March 10, 2013

ZIARA YA KINANA CHINA

Image
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) akimtambulisha Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema, kwa Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na Bashir Nkoromo). Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na  Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China. (Picha na Bashir Nkoromo). Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) akibadilishana mawazo na   Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika Machi 11, 2013, katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou, China.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA KOCHA ATHUMANI KILAMBO

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka baada ya kuongoza maelfu ya  waombolezaji katika mazishi ya  mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye  Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo  Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la  mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu  Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini  Dar es salaam. Marehemu Kilambo, ambaye alifariki jana usiku baada ya  kuugua saratani ya koo kwa takriban miaka miwili, atakumbukwa kama beki imara wa Yanga na Kocha stadi wa Pan Africa ambaye  aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 1982. Pia  amefundisha nyota wengi wa kandanda nchini wakiwemo kina Kassim Manara, Adolf Richard,  Mohamed Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao walichezea Taifa Stars kutokea Yanga na Pan. Rais Jakaya Mrisho Kikwete 

UJUMBE WA PONGEZI KUTOKA KWA RAIS WA TANZANIA KWA UHURU KENYATTA

Image
“Mpendwa Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kupokea taarifa ya ushindi wako wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu,  kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa  hakika, kwa niaba yangu binafsi kukupogenza kwa dhati ya moyo wangu kwa mafanikio haya makubwa ya kuchaguliwa kwako.” Ameongeza Rais Kikwete: “ Ushindi huu ni ushahidi na ishara ya wazi kabisa ya imani na matumaini ambayo wananchi wa Kenya waliyonayo katika uongozi wako. Huu ni  utambuzi wa kazi yako maridadi na mchango wako mkubwa  ambao umeutoa katika nafasi mbali mbali za uongozi katika  siku za nyuma katika jitihada zako za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ustawi wa nchi yako na wananchi wake.”  Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua madaraka ya juu zaidi katika nchi yako, napenda kukuhakikishia  msimamo wangu binafsi pamoja na ule wa Serikali yangu wa  kuunga mkono Serikali yako. Ni imani yangu kubwa  kwamba pamoja tutaweza kuendelea kusukuma m

Mh. Edward Lowassa aongoza harambee ya kuchangia miradi ya maendeleo Wilayani Butiama

Image
Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakiwasili kwenye hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Bodi ya Mradi huo,Dkt. Patrick Mugoya. Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache kabla ya kuanza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya usimamizi wa Padri Wojciech Adam (hayupo pichani)  wa kanisa Katoliki la Kiabakari lililopo wilayani humo,Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere  akizungumza machache wakati wa  hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo kat

TANZANIA YASAINI BILIONI 34.8 AFDB KUSAIDIA MIRADI YA MAJI ZANZIBAR

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah  (kushoto) akibadilishana hati na  Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero mara baada ya kusaini makubaliano leo jijini Dar es salaam ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) na  Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero wakisaini makubaliano leo jijini Dar es salaam ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar.

MARY RUTTA WA MANYARA ATWAA TAJI LA MISS UTALII TALENT 2013

Image
                 Mary na warembo wenzake wakishangilia ushindi huo.                    Mary Chrisostom Rutta, kutoka Mkoa wa Manyara (katikati) akifurahi baada ya kutangazwa mshindi. Kushoto ni Jamia Abdul (Kagera) na Joan John kutoka Lindi ambao waliingia tatu bora.               Warembo wakionesha vipaji kwa kucheza ngoma za asili. Wakionesha vazi la ubunifu.                  Msanii wa ngoma za asili kutoka Bagamoyo, Chemundu Gwao, akicheza na warembo hao. Mwakilishi wa Kagera, Jamia Abdul, akicheza ngoma ya Kihaya.                 Mikogo pia ilipewa nafasi yake mbele ya meza kuu.                  Rais wa Miss Utalii Tanzania na Jaji Mkuu wa kinyang’anyiro hicho, Gideon Chipungahero ‘Chipss’ (kulia) na majaji wenzake wakikusanya pointi.                   Meya wa Manispaa ya Temeke, Maabad Hoja, akimvisha Sasha mrembo huyo baada ya kutangazwa mshindi.                           DJ Max (kulia) na Mc Adria Cleophace walifanya kazi kubwa ya kunogesha tukio

KINANA AWASILI NCHINI CHINA NA UJUMBE WAKE

Image
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kulia) akizungumza na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano wa Kimataifa  ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming (kushoto) baada ya kuwasili leo Machi 11, 2013 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhu, kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku kumi nchini China. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai). (Picha na Bashir Nkoromo). NA BASHIR NKOROMO, CHINA Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewasili leo Machi 11, 2013 nchini China kuanza ziara ya kikazi ya siku kumi, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China. Kinana ambaye ni ziara yake ya kwanza kufanya nchi za nje tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa C CCM, Oktoba mwaka jana, amewasili akiambatana na ujumbe wa watu 14 wakiwemo viongozi na maofisa wa Chama na kupokewa  kwenye Uwanja wa Ndege wa Guangzhu, na  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano wa Kimataifa  ya Cha

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS JACKOB ZUMA JIJINI PRETORIA

Image
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini mwishoni mwa ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini humo ampapo alihudhuria mkutano wa vyama vilivyokuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika na pia aliongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC Troika jana(picha na Freddy Maro)