Mh. Edward Lowassa aongoza harambee ya kuchangia miradi ya maendeleo Wilayani Butiama



Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakiwasili kwenye hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Bodi ya Mradi huo,Dkt. Patrick Mugoya.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache kabla ya kuanza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya usimamizi wa Padri Wojciech Adam (hayupo pichani) wa kanisa Katoliki la Kiabakari lililopo wilayani humo,Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere akizungumza machache wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.ambapo Mgeni Rasmi katika harambee hiyo,alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari akitoa historia fupi ya mradi huo toka kuanza kwake mpaka walipofikia wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.ambapo Mgeni Rasmi katika harambee hiyo,alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono akizungumza machache wakati wa kukabidhi mchango wake na kuahidi kuendelea kuchangia ili kuhakikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara inafanikiwa huku akisikilizwa kwa makini na Mgeni Rasmi wa Harambee hiyo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono akikabidhi mchango wake kwa Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere huku akisaidiwa na Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimkaribisha Brigedia Jenerali,Zoma Kongo kukabidhi mchango wake kwa Mama Maria Nyerere kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara.
 Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono.
Rais wa Bodi ya Mradi huo,Dkt. Patrick Mugoya akizungumza machache kwenye hafla hiyo.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB