Posts

Showing posts from December 29, 2013

MAALIM SEIF ATEMBELEA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Image
Na Hassan Hamad, OMKR.  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Sharif Hamad, amesema serikali imepata moyo kuona taasisi, mashirika na wananchi jinsi walivyojitokeza katika maonesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.  Amesema kujitokeza kwao kwa wingi kunaashiria jinsi wananchi walivyohamasika kuonyesha na kutangaza huduma zao kwa wengine, kwa lengo la kuzitambulisha na kutafuta soko ndani na nje ya nchi.  Mhe. Maalim Seif ameeleza hayo baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya miaka 50 ya Mapinduzi yaliyoko Beit- el- Raas, mjini Zanzibar.  Amesema wananchi wameonesha kuyapenda maonyesho hayo ya bidhaa na huduma, na kwamba ni vyema yakaandaliwa kila baada ya muda, bila ya kusubiri miaka 50 mengine.  Maonyesho hayo ya kwanza ya aina yake kufanyika Zanzibar, yamekuwa kivutio kikubwa kwa wenyeji na wageni, yanazishirikisha taasisi mbali mbali zikiwemo taasisi binafsi, mashirika ya umma na wajasiriamali.  Katika ziara hiyo M...

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT. WILLIAM MGIMWA

Image
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Dkt. Mgimwa, Jane Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehe...

JK AMWAPISHA IGP MPYA NA NAIBU WAKE LEO IKULU

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii   Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam j...

USIKU WA TRADITIONAL FASHION SHOW WAFUNGA MWAKA KWA KISHINDO

Image
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Real Unique Tanzania, Bw. Albert Mkaoye ambao ndio waandaji wa Usiku wa Traditional Fashion Show akiwa kwenye red carpet na Mgeni rasmi MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin.  MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, na binti yake pamoja na wadau.

MAHFALI YA 9 CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR SUZA

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar  (SUZA) akimakabidhi zawadi Naibu Makamo Mkuu wa Chuo Taaluma Dk.Haji Mwevora Haji.kwa niaba ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Mzee Hassan Nassoro Moyo,wakati wa sherehe za mahfali ya 9 ya Chuo hicho katika kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Unguja jana,katikati Makamo Mkuu wa Chuo Prof Idriss Ahmada Rai.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar  (SUZA) akimakabidhi Cheti cha Ukutubi Miza Juma Makame,akiwa mwanafuzi Bora katika sherehe za mahfali ya 9 ya Chuo hicho katika kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Unguja jana,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar  (SUZA) akimakabidhi Che...

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AHUDHURIA JUBILEI YA KANISA KATOLIKI ARUSHA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Maaskofu wa Kaisa Katoliki baada ya Ibada ya Jubilei ya miaka 50 ya  Kanisa Kuu  la jimbo la Arusha  iliyofanyika mjini Arusha  Desemba 30,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

ZIARA YA DR SLAA TABORA KATIKA PICHA

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akikabidhi kadi ya chama hicho kwa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ngw'aluzwilo katika Kata ya Lusu jimbo la Nzega, baada ya mkutani wa hadhara kijiji ni hapo jana, akiwa katika ziara yake ya kujenga chama. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa akisalimiana na mbunge wa zamani wa jimbo la Bukene (CCM), Steven Kahumba, baada ya mkutano wa hadhara, uliofanyika Bukene juzi. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Nzega, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Setendi jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kujenga chama