Posts

Showing posts from February 3, 2013

JK awasili Dodoma leo kwa vikao vya CCM

Image
  Vijana wa CCM wakimvika skafu Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete muda mfupi baada ya kuwasili mjini Dodoma kongoza kukao cha Halmashauri kuu ya CCM taifa.   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM    Ndugu    Abdulrahman Kinana muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma ambapo ataongoza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM taifa.

MH FREEMAN MBOWE AKUTANA KWA DHARURA NA MKUU WA JUMUIYA YA ULAYA NCHINI

Image

Siku za Mwisho za uhai wake Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati Thomas Leizer Alikutana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo   (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless  Lema akibadilishana mawazo na Marehemu Thomas Leizer Hapa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la   Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati Thomas Leizer,  katika siku za mwisho za uhai wake, akiwa chumba cha uangalizi maalum  (ICU). Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless  Lema. Picha hii ilipigwa Jumapili ya wiki iliyopita, ambapo viongozi hao walifika kumjulia hali kiongozi huyo wa kidini aliyefariki jana mchana, baada ya kuugua kwa kuda mrefu na kulazwa katika Hospitali ya Selian  Hospital Arusha Centre.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA MAREKANI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo na Seneta, James Inhofe wa Jimbo la Oklahoma, wakati alipomtembelea Ofisini kwake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Seneta huyo jana Feb 6, 2013. Makamu wa Rais yupo nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc kwa ziara ya siku nne. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Johnnie Carson, wakati makamu alipofika Ofisini kwa Balozi huyo kwa mazungumzo leo, Feb 7, 2013. Balozi Carson ni msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Mfuko wa MCC, Daniel Yohannes, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kuhusu kuendelea kwa mradi wa MCC ii, nchini Tanznia. Mazungumzo hayo yalifanyika jana Feb 6, 2013 katika Hoteli ya Omni iliyopo Washngton Dc Marekani, ambapo Makamu yup...

TAIFA STARS YAICHAPA CAMEROON GOLI 1-0

Image
Mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon  Assou Ekotto  akimtoka mshabuliaji wa timu ya Taifa Stars katika mchezo wa Kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo Taifa Stars ikiibugiza timu ya Cameroon Goli 1-0  na kutoka uwanjani kifua mbele. Mchezaji wa timu ya Taifa Stars Salum Abubakar akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Cameroon Makoun Thierry katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo. Mashabiki mbalimbali wa timu ya Taifa Stars wakishuhudia mchezo huo ambapo Taifa Stars imeifunga Cameroon Goli 1-0. Wachezaji wa Taifa Stars wakishangilia mara baada ya  Taifa Stars kujipatia goli lake la kwanza na la mwisho lililofungwa na mchezaji Mbwana Samata. Ubao wa Matangazo ukionyesha matokeo ya mchezo huo. Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KUKUTANA NA RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE

Image
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's (wa tatu kushoto) na Ujumbe aliongozana nao kwa ajili ya mazungumzo na Rais Kikwete. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj, Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen ( wa pili kulia), Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka (wa pili kushoto) na wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's na ujumbe wake wakimsikiliza Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) alipohitimisha ziara yake kwa kumtembelea Ikulu jijini Dar. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. ...

Rais Jakaya Kikwete Amjulia Hali Mzee Msuya

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri Mkuu mstaafu,Mzee David  Cleopa Msuya aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili juzi jioni (picha Rashid Ngurungu-Ikulu)

Taswira : Kutoka Bungeni

Image

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma jana Januari 4, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuzindua  ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma jana Januari 4, 2013  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma jana Januari 4, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw Phillipe Dongier, wakifunua kitambaa cha jiwe la msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma jana Januari 4, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na viongozi wengine baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma jana Januari 4, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi mbalimbali wakipata maelezo juu ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma toka kwa mhandisi George Sambaliwakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndeg...

RAIS KIKWETE AKAGUA UJENZI WA DARAJA MTO MALAGARAS

Image