MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KUKUTANA NA RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE



Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's (wa tatu kushoto) na Ujumbe aliongozana nao kwa ajili ya mazungumzo na Rais Kikwete. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj, Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen ( wa pili kulia), Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka (wa pili kushoto) na wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's na ujumbe wake wakimsikiliza Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) alipohitimisha ziara yake kwa kumtembelea Ikulu jijini Dar.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's aliyemtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar jana. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's aliyemaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini baada ya kukutana na Rais Dkt. Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana tarehe 5, February, 2013.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni. (Picha zote na Zainul Mzige wa Mo Blog).

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB